Baada ya kuchoshwa na malalamiko ya jirani yake mnyamwezi Drake ameamua kukithibitisha kile alichokiahidi kwenye Ngoma “Where Ya At” ya mtu mzima Future.
Kwenye moja kati ya lines ambazo drake alisikika ni “I’ll buy the neighbors house if they complain about the noise Man”. Drake ameamua kuununua mjengo wenye thamani ya dola milioni 2.8 mali ya jirani yake mmoja ambae alizidi kulalamika kwa fujo ambazo drake amekua akizifanya anapokua mtaani kwake.
Mjengo huo wenye vyumba vine pamoja na mabafu 5 upo mita chache kutoka nyumbani kwa Drake.
Drake ambae alinunua nyumba mitaa hiyo mapema mwezi wa sita mwaka jana amefikia uamuzi huo ili aendelee kujiachia yeye na maisha yake kama alivyokaliliwa kwenye line nyingine ya ngoma hiyohiyo “Where Ya At” akisema “Cause nowadays I swear this shit done changed up for the boy
I’m self-made, selfish with my women, self-employed”
I’m self-made, selfish with my women, self-employed”
Ni Wazi Drake ameamua kuishi uhalisia wa kile alichokisema kwenye ngoma hiyo.