Haikua kuachia ngoma tu bali ilikua ni kuvunja rekodi ya muziki wa Afrika kwani tangu kuachiwa kwake hapo Juzi "Salome" imekua habari ya mjini,
Wimbo "Salome" uliimbwa na mwanamama Saida Karoli katika vionjo na Tamaduni za kabila la Kihaya umerudiwa na Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny umeendelea kuwa gumzo kwani katika hali isiyokua ya kawaida mashabiki wameendelea kusifu huku wengine wakitoleana mapovu kuhusu Diamond Kuirudia Ngoma hiyo.
ANGALIA BAADHI YA COMMENT ZA MASHABIKI:
Video ya Salome huenda ikatajwa kuwa video ya Kiafrika iliyotzamwa mara nyingi ndani ya muda mfupi kwani tangu kuwekwa kwake kwenye mtandao wa YouTube siku mbili zilizopita tayari imeangaliwa zaidi ya mara Laki sita.