Mixtape yake
aliyoipa jina la “Jeffery” ambayo iliingizwa rasmi sokoni tarehe 25, 08 mwaka
huu imemfanya Young Thug Kuvunja recodi ya Billboard kwa kuingiza rekodi ya kushika nafasi za juu kwa albamu tatu tofauti kwenye chati mbalimbali.
“Jefferry”ambayo iliingia kama namba nane
kwenye Billboard Top 200 imetajwa kuuza kopi 37,000 ndani ya wiki yake ya kwanza.
Mapema mwezi Februari mnyamwezi Young Thug aliachia Mixtape "I'm Up" ambayo iko nafasi ya sita, iliuza kopi 15,000 kwenye wiki yake ya kwanza iliyofuatiwa na "Slime Season 3" ambayo nayo kwenye wiki yake ya kwanza iliuza kopi 22,000.
Artwork
ya mixtape Jaffery ambayo inamuonyesha
mtu mzima Young Thug akiwa amevaa gauni ni stori kubwa amabayo iliwafanya watu
wengi kuwa na maswali mengi kwa Young Thug huku wengine wakidai ameharibikiwa
“Linapokuja suala la swagga hatujali jinsia
gani wanapendeza mavazi gani” aliswahi kuongea Young Thug kwenye moja ya
Interview zake. “Nikiliona lile gauni huwa nahisi ni kama Mungu ndie
alinipatia” aliongeza Young Thug.
Young Thug
pia alikiri kuanza kuvaa nguo za kike tangu akiwa na umri mdogo na hajawahi
kuwa na matatizo yeyote ya kijinsia.
“Nilipokua
na miaka 12 miguu yangu ilikua midogo sana hivyo nilikua napenda kuvaa viatu
vya dada zangu” Ilifika hatua baba yangu alikua anakasirika kiasi cha kunizuia
kutoka kokote kwa kudai nitamuaibisha lakini mimi sikuwa naikijali watu
wataongea nini”