Friday, October 14, 2016

Homa ya Kimeta yahofiwa kuingia nchini.


 WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imesema ugonjwa ulioua watu wawili na wengine wanane kulazwa katika Hospitali ya Enduleni ndani ya Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro unaweza kuwa ni 'Kimeta'.

Hayo yalibainishwa   Dar es Salaam jana katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu  ya Sekta ya Mifugo, Dk. Maria Mashingo,hii ikiwa ni siku mbili baada ya kuripotiwa kuwa ugonjwa wa 'Sotoka' umeua watu wawili na nane  kulazwa.

"Ugonjwa huo uliripotiwa kwa makosa, ambao umesababisha athari za  afya ikiwamo vifo vya watu wawili na wanane kulazwa hospitalini unaweza kuwa ni kimeta ambao ndiyo ugonjwa wa wanyama unaoathiri binadamu na upo maeneo ya Wilaya ya Ngorongoro"..."Ugonjwa wa Sotoka kwa Ng’ombe unajulikana kitaalamu kama ‘rinderpest’ na kwa mbuzi na kondoo unajulikana kama ‘Peste Des Petirs Ruminants’ (PPR) ni ugojwa ambao kwa ng’ombe nchini tulishaitokomeza,".Alisema Dk Maria.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuchukua tahadhari ya kula nyama iliyokaguliwa na wataalamu wa mifugo na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.