Baada ya kolabo yake ya 'One Dance' aliyoshirikishwa na rapper mzaliwa wa Toronto,Canada, Drake kufanya vizuri,Mkali wa miondoko ya Pop kutoka nchini Nigeria,Wizkid yupo mbioni kuachia kazi nyingine ya kwake akimshirikishwa Drake ambae amechaguliwa kuwania vipengele 11 kwenye tuzo za American Music Awards.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter,Wizkid ameandika;
"Just know i'm about to release some of the best works i've ever".." "6god x Real Starboy about to school everybody!!".Zilisomeka Tweet hizo za Wizkid.
Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya muziki wanadai kuwa huenda jina wimbo huo aliofanya na Drake,"Real Star Boy" huenda ni kijembe kwa Mwanamuziki The Weekend ambae mwezi Septemba mwaka huu aliachia wimbo unaofahamika kama "Star Boy",unaopatikana kwenye album yake mpya inayofahamika kama "Everybody's a Star" album ambayo bado haijafahamika tarehe ya kutoka kwake,ambapo pia jina la wimbo huo yaani 'Star Boy' ni a.k.a ya Wizkid ambae lebo yake ya muiziki inafahamika kwa jina hilo pia.
Mbali na kushirikishwa na Drake kwenye kolabo ya 'One Dance',Drake aliurudia wimbo wa Wizkid 'Ojoulegba' ambapo ndani yake pia alisikaka rapper Skepta na kumfanya Wizkid kutambulika kwenye mataifa mbalimbali ya magharibi.