Tuesday, October 11, 2016

Mahakama yamrejesha kazini aliefukuzwa kazi Benki Kuu miaka 22 iliyopita,aelezea mateso aliyopitia.




Dar es salam.Haikua kazi rahisi,Miaka 22 ya wafanyakazi 31 wa Benki kuu ya T anzania (BOT) kutafuta haki yao wakigubigwa na umasikini,maradhi na vuta nikuvute ya migogoro ya kishereia.

Hatimae haki hiyo imepatikana Oktoba 2 mwaka huu baada ya Mhakama ya Rufani kuwarejesha ikisema walifukuzwa kazi mwaka 1993 bila kufuata sheria.

Kiongozi wa Wafanyakazi hao Samson Magoti aliyesimamia kidete kuhakikisha wanapata haki yao ameelezea maisha magumu aliyopitia katika kipindi hicho ikiwamo kuugua kiharusi kutokana na mawazo na kukimbiwa na mke.

"Haikua kazi rahisi,lakini hatimae Mahakama imetenda haki na kama si majaji wanaosimamia maadili ya kazi yao,leo pengine tusingepata haki yetu,".Alisema Magoti.

Mazungumzo haya na Magoti yalifanyika nyumbani kwake,Yombo Dovya,Wilayani Temeke tulimpomkuta yeye na familia yake ya watoto wanne kati ya sita,mke (mwingine) na Mama yake mzazi,ajuza wa miaka 102.

Tulipofika nyimbani kwake,alitukaribisha kwenye banda la uani ambalo baadae alitueleza kuwa lilikua likitumika kufugia kuku lakini kutokana na ugumu wa maisha,sasa ndiyo makazi ya familia hiyo ambapo robo ya banda hilo limejengwa kw matofali  na robo tatu iliyosalia ni maboksi (ceiling board).

Tullipowasili nyumbani kwake,mke wa sasa wa Magoti,Naomi Samson alikua akijiandaa kwenda kuuza ufuta katika Shule ya Msingi Buguruni na alipotukaribisha,tuliuliza bei ya ufuta nae alitujibu:"Huu ni sh.100,una Bluetooth,Whatssap na Memory card".

Alisema miaka miaka mitatu tu,baada ya kufukuzwa kazi,migogoro ilianza kwenye ndoa yake,mkewe alibadilika nae akawa hana sauti ndani ya nyumba.

"Kama huna kazi unakua mnyonge,huna sauti,kwa sababu kila unalomwambia atakujibu atakavyo na atasingizia anatafuta hela na wewe kweli huna".Baada ya migogoro hiyo mkewe aliondoka na kumuachia watoto watatu.

Chanzo:Mwananchi.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.