Mchekeshaji kutoka nchini Kenya Eric Omond amefanya kituko kingine mbele ya mpenzi wake ambae ni raia wa Italia Chantal Graziol.
Ishu nzima ilianzia wakati mrembo huyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akitokea kwenye ziara ya maenesho ya mitindo barani ulaya,ambapo Eric alimpokea mpenzi wake akisindikizwa na kikundi cha ngoma cha 'Masai Dance'.
Mchekeshaji huyo aliejipatia umaarufu nchini kutokana na aina yake ya uchekeshaji wa kuigiza maisha ya watu maarufu,hakuishia hapo kwani alimzawadia mpezi wake gari jipya lililokua uwanjani hapo tayari kwa kuwapeleka nyumbani.Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika; “Mungu akileta bibi analeta na Gari yake MyBabysNewBaby”.