Monday, October 10, 2016

MDAHALO WA URAIS MAREKANI:Skendo za familia zaibuliwa kwenye mdahalo wa Donald Trump na Hillary Clinton.

Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican Donald Trump alipokua akirudi Jukwaani St Louis kwa mjadala wa pili kati ya mitatu iliyopangwa, hakupeana salamu ya kushikana mikono na Mgombea wa chama cha Democratic Bi.Hilary Clonton jambo lililodhihirisha chuki ambayo ingeendelea katika kipindi kizima cha mjadala huo.


Donald Trump alitangualia kwa kutetea matusi aliyotoa kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu za siri kwa kumshambulia Hillary Clinton na familia yake hasa mumewe.

Mgombea huyo wa chama cha Republican, amekana kamwe kutowanyanyasa wanawake kingono huku akipeleka  hasira zake kwa aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton katika majibizano makali kwenye mjadala huo.

"Hakuna mtu katika historia ya siasa ambaye amewanyanyasa wanawake kiasi hicho," alisema.
Hillary Clinton ambae alikataa kujibu tuhuma dhidi ya mumewe.

Matamshi ya bwana Trump dhidi ya familia ya Bi. Clintons yalijiri baada ya muendesha mjadala Anderson Cooper kumuuliza kuhusu kanda ya video ya mwaka 2005 iliyosambazwa katika vyombo vya habari Ijumaa iliyomfichua Trump akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu zao za siri ambapo  alipoendelea kuulizwa kuhusu iwapo alimnyanyasa kingono mwanamke yoyote, alikana kufanya hivyo na badala yake akamulika tuhuma zilizomuandamana Bill Clinton katika siku za nyuma.

Wagombea hao wawili walizozana kuhusu mzozo wa Syria, Uchokozi wa Urusi, na hatua ya bwana Trump kukata kutangaza malipo yake ya kodi na mpango wake wa ukaguzi mkali kwa wahamiaji wanaowasili kutoka mataifa yanayohusishwana ugaidi.

Hatimaye mjadala ulikamilika wakati mwanamume mmoja kutoka umati uliokusanyika kufuatilia mjadala huo, alipowauliza wagombea hao wawili kusema kitu kimoja kizuri kumhusu mwenzake ambapo  Hillary Clinton alisema watoto wa Trump wanamdhihirisha ni mtu wa aina gani huku Trump akamtaja mpinzani wake kuwa mpiganaji  asiye kata tamaa.
-BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.