Wednesday, October 12, 2016

Mtandao wa Amazon wazindua huduma ya kuuza na kusikiliza muziki mtandaoni.


Mtandao wa Amazon umeamua kuingia rasmi kwenye biashara ya kuuza na kusikiliza muziki mtandaoni,wakitarajiwa kuleta ushindani na mitandao mingine maarufu kwenye biashara hiyo kama  Spotify's na Apple Music.

Huduma hiyo inayoitwa Amazon Music Unlimited  (Amazon Music Unlimited) , inapatikana kwa kiasi cha $7.99 kwa mwezi kwa wateja wa mtandao wao ikiwa ni pungufu ya kiasi cha $9.99 kinachotozwa na mitandao ya Spotify's na Apple Music.


Huduma hiyo imeingiza Mtandaoni jumla Nyimbo milioni 10 kutoka sehemu mbalimbali Ulimwenguni,wakiwa kwenye ubia  na lebo kubwa za muziki kama Sony,Universal na Warner Brothers.

Kwa sasa huduma hiyo inapatikana nchini Marekani,ikitarajiwa kutambulishwa kwenye mataifa mengine kama Uingereza,Ujerumani na Austria baadae mwaka huu.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.