Facebook imenzisha mfumo mpya wa
mtandao unaojulikana kama Workplace, ambao utaziwezesha kampuni kubuni
njia ya kufanya mawasiliano.
Mtandao huo unaofanana na wa
Facebook, na ulio na sehemu muhimu zikiwemo za kuonyesha video live na kwa mawasiliano ya ujumbe, hauwezi kutumiwa na mtu binafsi.Mtandao huo umebuniwa kuchuchukua mahala pa mifumo mingine kama ya email kwa mawasiliano kazini.
Mdadisi mmoja alisema kuwa mtandao huo utatoa ushindani mkubwa kwa mifumo mingine washindani.
Utaingia kwenye masoko sawa na ya mtandao wa Microsoft wa Yammer, ambao makampuni yanaweza kutumia na ule wa Slack ambao ni wa mawasiliano ya ujumbe.
Facebook imekuwa ikiufanyia majaribio mfumo huo ambao awali ulifahamika kama Facebook at Work, kwa muda wa miaka miwili na kusema kuwa hadi makampuni 1000 tayari yanautumia.