Wednesday, October 12, 2016

Msemaji wa Donald Trump adai Wanamuziki wa HipHop ndio wahamasishaji wa matukio ya ubakaji,ajibiwa mitandaoni na mastaa wa muziki huo.


Msemaji wa mgombea Urais wa Marekani Dolnald Trump,kwa tiketi ya chama cha Republican Katrina Pierson aliwashangaza watazamaji kwenye mahojiano na kituo CNN interview   ,Mara baada ya kudai kuwa Wanamuziki,hasa wa HipHop nchini humo ndio wanaohamasisha matendo ya ubakaji kwenye jamii kupitia nyimbo zao,Hii ikiwa ni baada ya kutakiwa kuelezea vitendo vya udhalilishaji vidavyodaiwa kufanywa na Bwana Trump baada ya video zake akiwadhalilisha wanawake kusambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita.


 “This rape culture is purported by none other than the entertainment industry, none other than Hip Hop music, which you can hear on local radio stations.” .Alisema

 Hata hivyo Muongozaji wa kipindi hicho Carol Costello alimkatisha na kumtaka afafanue tuhuma za Bwana Trump ambae anachuana vikali na mgomea wa chama cha Democratic,Bi.Hillary Clinton.


Hatua imekuja baada ya Wanamuziki wengi wa HipHop kumpinga Bwana Trump kutokana na matamshi yake tata kuhusu masuala ya uraia hasa kwa raia wa Marekani wenye asili za mataifa mengine.

Baadhi ya Wanamuziki hao walishindwa kuficha chuki zao dhidi Bwana Trump kwa kumbeza  mitandaoni mara baada ya kumalizika kwa mdahalo wa pili wa Urais kati yake na Bi.Hillary Clinton mapema mwezi huu.





 

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.