Sunday, October 23, 2016

PICHA / VIDEO:DJ Khalid na mpenzi wake wapata mtoto wa kiume,aweka video ya 'baby mama' akijifungua 'Snapcharts'.




 Mtayarishaji wa muziki DJ Khalid na mpenzi wake wa siku nyingi Nicole Tuck wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume huku akionesha tukio zima la kuzaliwa kwa mtoto wake kupitia mtandao wa 'Snapchart'.

DJ Khalid na Nicole Tunk.


Khalid ambae ni balozi wa mtandao wa 'Snapchart' alipost video kwenye mtandao huo akielezea furaha aliyonayo juu ya ugeni huo kwenye familia yake huku akitokwa na machozi ya furaha.



Hakuishia hapo tu,bali ili-post video nyingine ikimuonesha daktari akimchora kwa wino mchoro wa unyayo wa mtoto wake kwenye mkono wake na kuandika, "I love you son!!!'



Dj Khalid ambae amejijengea umaarufu mkubwa kwenye muziziki wa 'Hip Hop' kupitia lebo yake ya muziki ya 'We The Best Music' katika kipindi cha muongo mmoja sasa,album yake ya 'Major Key' iliyowajumuisha mastaa wakubwa wa muziki nchini Marekani kama,Jay Z,Nas,J Cole,Future na wengine wengi imempa mafanikio makubwa kwenye mauzo yake na kufika  namba moja kwenye chati maarufu za 'Billboard'.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.