Simu ya kampuni ya Samsung aina ya
Galaxy Note 7, ambayo awali ilithibitiishwa na kampuni hiyo kuwa
ilikuwa salama, imezua taharuki baada ya kushika moto kwenye ndege nchini Marekani.
Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake ambapo Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.
Mmiliki wa simu hiyo Brian Green, akizungumza na Jordan Golson wa shirika la The Verge, amesema alinunua simu hiyo tarehe 21 hii ikiwa ni baada ya Sumsung kuzirudisha sokoni simu mpya za Sumsung Gulaxy Note 7 ikiwa na alama ya mraba ya rangi nyeusi kwenye pakiti yake, alama ambayo iliongezwa na Samsung kutofautisha kati ya simu zilizokuwa zimeuzwa awali ambazo zilidaiwa kutokuwa salama na kuongeza kuwa,Mara baada ya simu hiyo kushika moto aliitupa nnje kupitia dirishani.
"Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwa simu. Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege." .Msemaji wa Shirika la ndege la Southwest Airlines aliiambia BBC.