Thursday, October 6, 2016

"Scopion",anaedaiwa kumtoboa mtu macho afanya vituko mahakamani.

Salum Henjewele (34) maarufu kama "Scorpion" mkazi wa Yombo Machimbo anaetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho Said Mrisho jana aliwashangaza watu mara baada ya kufanya vituko mahakamani alipokua akisomewa mashtaka yanayomkabili.

Scopion ambae ni mwalimu wa mchezo wa mashwati (karate) alimfanyia unyama huo Said mnamo Septemba 6 mwaka huu eneo la Buguruni Sheli Jijini Dar es Salaam.


Katika hali ya kushangaza,mtuhumiwa huyo alibadilisha mavazi yake akiwa Mahakamani ili asijulikane mbele ya umati wa watu waliokua wamefurika Mahakamnii hapo.Akiwa anatoka mahakamani Scopion alionekana amevaa mavazi tofauti  na yale aliyokua amevaa asubuhi wakati kesi yake ilipokua ikitajwa.

Awali Scopion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore  kwa kuongozwa na wakili wa serikali  Munde Kalombola na kumsomea mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kumsababishia upofu wa kudumu Said Mrisho kwa kumtoboa macho.

Hata hivyo shauri hilo limeahiriishwa hadi Oktoba 19 mwaka huu litakapotajwa tena ambapo kwa mujibu wa hati hiyo ya mashtaka ya kesi hiyo namba 276 ya mwaka 2016 ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 28 mwaka huu ambapo hata hivyo wakati akisomewa mashtaka yake yake,mtuhumiwa huyo alionekana mtu asiye na wasiwasi huku akitabasamu muda wote.

Inadaiwa kuwa mnamo Septemba 6 mwaka huu majira ya saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli,Manispaa ya Ilala,Dar es salaam,mtuhumiwa aliiba cheni ya silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh.60,000 na "black bend" ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh.330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh.474,000 mali ya Said Mrisho aliemtia upofu kwa kumtoboa macho,ambapo wakali wa serikali aliongeza kuwa kabla kutekeleza tukio hilo mtuhumiwa alimjeruhi Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo machoni,tumboni na mabegani ili kurahisishwa kupora mali hizo.

Mama mzazi wa Mrisho;

Nje ya mahakama hiyo,mashuhuda wa Shirika la Wambea Duniani,(Shilawadu) walimuona mama mzazi wa mrisho aitwaye Halima Jissu pamoja na ndugu na jamaa zake wakilia muda wote huku wakisema wanamwachia Mungu kwa kilichotokea.




Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.