Tuesday, November 1, 2016
Boniface Jacob (CHADEMA) ashinda nafasi ya Umeya Ubungo.
Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob ameshinda nafasi ya Umeya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo baada ya ule wa awali kuhairishwa.
Amepata ushindi wa jumla ya kura 16 za UKAWA na kura 2 CCM huku Naibu Meya akishinda kwa kura 15 dhidi ya kura 3.
Uchaguzi huo umefanyika baada ya kuundwa kwa Manispaa mpya ya Ubongo iliyokua ndani ya Manispaa ya Kinondoni ambayo Jacob awali alikua Meya wa Manispaa hiyo.
Comments System
facebook