Wednesday, October 5, 2016

Wiz Khalifa na mwanae kutambulisha mavazi yao mapya.


 Rapper Wiz Khalifa ameamua kuingia kwenye ulimwengu wa mitindo ambapo anatarajia kuitambulisha "Clothing line" ya mavazi yake inayofahamika kama "BUSH" sambamba na mwanae wa kiume Sebastian chini ya kampuni tanzu ya mavazi inayofahamika kama Junk Food Clothing.


Wiz Khalifa amedai kuwa amehamasika kubuni aina hiyo ya mavazi kutokana muonekano wa mwanae ambae kwa muda mrefu amekua akimvalisha mavazi ambayo anahisi yamemtengenezea muonekano tofauti hivyo kuamua kuingiza sokoni aina hiyo ya mavazi ambayo itakua maalum kwa watoto na wazazi wao hasa wazazi wa kiume kama ilivyo kwake na mwanae Sebastian aliezaa na aliekua X-Girl wake,Mwanamitindo Amber Rose.


 "All the designs are based around Sebastian"... "I just really wanted it to feel personal to him, so when he sees it, he gets excited. He’s 3 years old, so he might not understand the concept of having his own clothing line. But the fact that all of his favorite things are all over his clothes, it makes him feel special; it makes him entertained by what he’s wearing." .Wiz Khalifa aliumbia mtandao wa PEOPLE.
 Aina hiyo ya mavazi inajumuisha T-Shirt,Sweatshirt pamoja bidhaa nyingine za mitindo ambapo kwa watoto mavazi hayo yatauzwa kwa kati ya kiasi cha $35 hadi $50 ambapo kwa watu wazima yatauzwa kwa kati ya kiasi cha $45 hadi $80.Mavazi hayo yanatarajiwa kuzinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.