Amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wa kujipumzisha, "hazifai kwa mtu wa hadhi yake" hivyo kuwaomba radhi mashabiki wa soka nchini humo hii ikiwa ni baada ya gazeti la The Sun la Uingereza kuchapisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney, 31, akiwa amelewa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.
Hata hivyo Rooney hakucheza mechi ambayo Uingereza walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti.

