Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Riverside jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa
Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa
kabla ya kufika Machi mwakani.
Kauli hiyo aliitoa kwenye ibada ya Jumapili ya tarehe 11 ya mwezi Disemba 2016,ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne
katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya
habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake,huku akidaiwa kufanya kitendo hicho akiwa amelewa.
“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai,
mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu
ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata
leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.
Chanzo:Mwananchi.