Sunday, December 11, 2016

EATV AWARDS-2016:HIZI NDIZO FIGISU ZA TUZO YA VANESSA MDEE KUPEWA LADY JAY DEE..!?


Kwa mara ya kwanza kituo cha Televisheni cha EATV kiliandaa na kuratibu utoaji wa tuzo kwa wasanii nchini katika hafla iliyofanyika jumamosi ya tarehe 10 Disemba 2016 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam,Hii hatua kubwa kwa chombo cha habari kutambua mchango wa sanaa na wasanii ambao kupitia kazi zao vyombo vya habari vimekua vikijozolea wasikillizaji na watazamaji kupitia vipindi vyao hivyo EATV wanastahili pongezi sambamba na kuungwa mkono kwani utoaji wa tuzo sio tu huongeza ari kwa wasnii wetu bali tuzo ni kipimo cha maendeleo ya sanaa kuanzia kwa msanii mwenyewe na sanaa kwa ujumla.Ni aibu mpaka mwaka unaisha tuzo maarufu za Kilimanjaro Music Awards (KTMA),hazijafanyika na wala hakuna taarifa yoyote rasmi ya kutofanyika kwa tuzo hizo,hii ni aibu kubwa sana kwa Baraza la sanaa nchini BASATA ambao ndio waratibu wakuu wa tuzo hizo.


Tuachane na mambo ya BASATA maana nadhani wanachojua ni kuzifungua nyimbo na kuwapiga wasanii faini.Kwa upande wa tuzo za EATV,nawapongeza waandaji kwa ubunifu wao japo tuzo hizo zilitolewa kwa mara ya kwanza.Kila kitu kizuri hakikosi kasoro na tusisahau kasoro zikitazamwa kwa jicho pevu ni sehemu ya kujikosoa,kujitathimini na kuongeza ufanisi,hivyo basi sina tatizo na Ali kiba kuwa kinara wa tuzo hizo kwa kujinyakulia jmla ya tuzo  3 bali nna shaka na ushindi wa Mwanamama,Komando Lady Jay Dee kama mwanamuziki bora wa kike.Sina tatizo na kipaji cha Jide ambae hata mimi ni shabiki wa nyimbo zake ila tukubali tukatae nadhani majaji na waratibu wa tuzo hizi au kwa kujua,kwa kutojua au kwa kusudia wameteleza kwa kutompa Vanessa Mdee tuzo hii hasa ikizingatiwa namna Vanessa Mdee alivyoitangaza nchi yetu kwa nafasi yake kama Mwanamuziki wa kike kutoka Tanzania hadi ubalozi wa Marekani nchini kumchagua Vanessa kuwaongoza mabinti kwenye mdahalo wa kampeni ya elimu kwa watoto wa kike duniani,mdahalo ambao uliongozwa na mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama.

Sitaki niwachoshe na maneno mengi,ila kwa mwaka huu Jide alikua na 'Hit songs' ngapi..? 'Ndi Ndi Ndi','Sawa na Wao' eheee we unaijua nyingine...okey,twende kwa Vanessa,'No Body But Me' aliyofanya na rapper K.O,'Pale kati',bado colabo zake na Navy Kenzo,Mwana Fa,G.K kundi la Weusi bila kusahau colabo yao na X-Boy wake Juma Jux inayofahamika kama 'Juu', hapo hatujazungumzia video yake mpya ya 'Cash Madam' aliyoamua kufunga nayo mwaka.Tusisahau nyimbo zake sio tu zimesumbua kwenye chati za muziki nchini bali hadi kwenye chati za vituo mbalimbali vy kimataifa kama MTV,TRACE MUSIC nk.

Vanessa ametumika na makampuni mangapi mwaka huu kwenye matangazo,kwanini wanamtumia..?,Hata Coke Studio walimpa dili kwa mara ya pili kwenye msimu wa shoo yao ambapo aliungana na mastaa wakubwa ulimwenguni kama Trey Song kutoka nchini Marekani.Tazama FOX Televisheni moja ya vituo vikubwa vya TV ulimwenguni,kila baada ya muda utamuona Vanessa akiwa na kina Patoraking na Casper Nyovest  kwenye promo za vipindi vya Afrika,sasa tujiulize kwanini wanamtumia Vanessa,tukubali au tukatae,EATV wamepuyanga kama wanavyosema watoto wa mjini kwa kumnyima tuzo V- Money na kumpa Lady Jay Dee,japo sijajua msingi wa kumpata mshindi ulikua ni kwa kura pekee
Ila ukweli ni kuwa waliotajwa kuwania kipengele hawakua na vigezo vya kumpokonya tuzo hii Vanessa kwa mwaka 2016 kutokana na juhudi zake za kurudisha heshima kwa Wanamuziki wa kike juhudi ambazo hata Komando Jide kwa miongo kadhaa sasa amekua akizifanya kupitia muziki wake.Kama kweli wewe ni mpenzi wa sanaa na unaufatilia muziki unadhani kwa mwaka 2016 Jide,Linner,Ruby na Lilian Mmbabazi kutoka nchini Uganda waliokua wakiwania kipengele cha Mwanamuziki bora wa kike yupi alistahili kupea tuzo hii..?

Hawa ni washindi wa tuzo za EATV AWARDS-2016.



1. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume 2016 kimekwenda kwa Ali Kiba.
2. Wimbo wa Aje wa Ali Kiba umeshinda tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2016.
3. Video ya wimbo wa Aje ya Ali Kiba imeshinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka 2016.
4. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike 2016 kimekwenda kwa Lady Jay Dee.
5. Tuzo ya Heshima inayotolewa kwa mtu/taasisi yenye mchango mkubwa katika sanaa ya Tanzania inakwenda kwa Dj Bonny Love.
6. Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka 2016 imekwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu ya Gabo Zigamba.
7. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume 2016 inakwenda kwa mwigizaji Salim Ahmed maarufu Gabo Zigamba.
8. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike 2016 inakwenda kwa mwigizaji Chuchu Hans.
9. Navy Kenzo wameshinda tuzo ya Kundi Bora la Muziki 2016.
10. Mwanamuziki Man Fongo ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi 2016.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.