DAR ES SALAAM-Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo mapema leo amefikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa mashtaka matatu likiwemo shitaka lakuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao. kati ya mashtaka hayo,mawili amepata dhamana huku la tatu likiendelea kuwa kizungumkuti cha Bwan.Melo kukosa dhamana.
Mawakili wanaomtetea wanaendelea kushughulikia dhamana ya mteja wao ambae tayari anaidaiwa amepelekwa gereza Keko.
HIZI NI HATI ZA MASHTAKA
Kwa siku tatu mfululizo Jeshi la Polisi lilimshikilia Melo ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media inayomiliki mtandao wa 'Jamii Forum',akitakiwa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.