Wednesday, December 14, 2016

Mfahamu Edward Snowden,Jasusi wa CIA anaemuumbua Obama na ushahidi kuwa Osama Bin Laden yupo hai.


1481465176989.jpg

EDWARD SNOWDEN alizaliwa mjini North Carolina June 21,1983, babu yake (upande wa mama alikuwa admeri (Afisa darala la kwanza katika jeshi la majini) ambae baadae akawa afisa wa juu wa Shirika la kijasusi la Uingereza (FBI), bahati mbaya alikua mmoja wa wahanga wa mlipuko wa Pentagon 9/11. Baba'ke alikuwa mlinzi wa fukwe/pwani (Coast guard), mama'ke alikuwa msaidizi mkuu (chief assistance) mahakama ya jimbo la Maryland. Dada'ke alikuwa mwanasheria wa serikali. Akiwa katika umri mdogo kabisa (13), Snowden alipata alama zaidi ya 150 katika mitihani miwili ya kipimo cha IQ. Akiwa mdogo alipata ugonjwa aliomsababisha asiende shule takriban miezi 10, aliporudi shule alikuta mitihani ya GED akaifanya na kufaulu  kwa wastani wa juu sana. Japo hakupata Bachelor degree, alifanikiwa kupiga Master's ya chuo kikuu cha Liverpool, Uingereza mwaka 2011. Akiwa na miaka 20 alitaja Ubudha (Buddhism) kama dini yake katika fomu za kujiunga na jeshi.

MTAZAMAO WA KISIASA WA SNOWDEN:

Snowden anadai kua uchaguzi wa 2008 (uliomweka Obama madarakani) alimpigia kura mgombea wa chama cha tatu (3rd-party candidate). Hakuamini katika falsafa za Obama na anadai kwamba alipanga avujishe siri za kijasusi za Nationa Security Agency (NSA) tangu 2009, lakini aliona busara avute subira akiamini kua Obama angetekeleza ahadi zake tofauti na Bw. G. W. Bush.

Baada ya kuvujisha siri nzito za kijasusi na usalama wa Marekani mwaka 2013, jukwaa la kijamii la Ars Technica lilithibitisha kuwa Snowden alikua active member wa jukwaa hilo na kwamba mwaka 2009 katika uzi unaohusu kulinda usalama wa taifa, Snowden alipost kwamba "I think leakers of classified information should be shot in the balls"-- "Nafikiri kwamba wavujishao siri nzito za taifa wapigwe risasi za korodani".

AJIRA:
May 2004, Snowden akiwa na miaka 21 aliorodheshwa kwenye kikosi cha akiba (US Army reserve). Alitamani sana kupigana vita ya Iraqi akiamini kwamba kupigana vita hivyo ni ishara ya ukombozi kwa watu wanyanyaswao, bahati mbaya hakufanikiwa kwakua alivunjika miguu akiwa kwenye mafunzo ya kijeshi.

2005 aliajiriwa kama mtaalamu ya maswala ya usalama katika chuo cha Maryland. Mwaka 2006 aliombwa ajiunge na CIA, ambapo aliwekwa kitengo cha mawasiliano ya kimataifa na upelelezi wa mtandao (network surveillance) makao makuu ya CIA Virginia. Mwaka huo alipost kwenye jukwaa la Ars Technica kuwa "siwezi kuhangaika kutafuta/kupata ajira kwakuwa mimi ni mchawi wa kompyuta", akiwa kijana mwenye umri mdogo zaidi katika timu ya wataalamu wa usalama wa mtandao, alipelekwa masomoni katika shule ya siri ya CIA kwajili ya kupata utaalamu wa hali ya juu ya kompyuta, ambapo aliishi hoteli yenye hadhi ya nyota 5 mwaka mzima akipata mafunzo hayo maalumu.

1481467089300.jpg

Mwaka 2007, CIA walimwagiza Snowden aende Geneva, Uswisi pamoja na jopo la wanadiplomasia kwajili ya kuchunguza na kuoperate usalama wa mtandao wa vikao vya siri. Alipewa pasi ya kusafiri ya Marekani daraja la diplomasia na alikabidhiwa apartment ya vyumba vinne karibu na ziwa Geneva. Akiwa kwenye hiyo trip, Snowden alishuhudia kwa macho jinsi CIA walivyoweza kuwahonga kwa rushwa kubwa mno maafisa wa benki ya dunia, maafisa wa ulinzi na wanasheria ili CIA waweze kujua siri za ndani za World Bank. Snowden alipigwa butwaa, kivipi Marekani ilikuwa inahubiri uwazi na kupinga vikali rushwa lakini kumbe ndani ya tundu la sungura wao wanatenda kinyume. Snowden alikasirishwa mno na tukio hilo.
Mwaka 2008 Snowden alichaguliwa na CIA aongozane na raisi Obama katika mkutano wa NATO huko Romania.ambapo mnamo Feb 2009, Snowden alimua kujiuzulu kua agenti wa CIA tayari akiwa na siri nyingi sana za ndani. 1481467813123.jpg

March 2009, alianza kazi kwenye kampuni binafsi la Dell ambapo alikua na wajibu wa kutoa maelekezo juu ya kuhakikisha usalama wa mitandao ya wateja wa Dell kuepuka cyber attack. Wateja wa Dell wakubwa walikuwa Yokota Air Base, Shirika la kijasusi la China, mashirika ya serikali na wizara mbali mbali za Marekani, CIA pamoja na kusimamia mifumo ya mawasiliano ya National Security Agency.
1481468111514.jpg

Upelelezi wa kitaalamu unaonesha kwamba Akiwa Dell, kuanzi April 2012, kwa kutumia ujuzi wake wa hali ya juu ya kompyuta, Snowden alianza rasmi kupakua mafaili ya siri za kiusalama za marekani ambazo inakadiriwa kufika zaidi ya documents million 1.

Akiwa analipwa mshahara wa mil. 420 tsh kwa mwezi, Snowden aliamua kuacha kazi katika kampuni ya Dell. Alikua na msukumo wa kumwaga siri zilizomchukiza za usalama wa dunia, lakini alisubiri apate pa kuanzia "breaking point". Siku ambayo kiongozi mkuu wa NSA Alipolidanganya Bunge la marekani (congress) na kula kiapo feki ndipo ilikuwa breaking point yake.

Mwezi mmoja baadae alitoroka marekani kuelekea Urusi ambapo alipewa hifadhi ya maficho (asylum) na Raisi Vladimir Putin. Baada ya kujihakikishia kuwa ana ulinzi imara ndipo Snowden alipoanza kurusha makombora kupitia mtandao wake maarufu wa Weakleaks.com,mtandao ambao umefungiwa nchini Marekani huku ukiwa na sifa ya kuandika habari nyeti zinzowahusu viogozi na watu mashuhuri Ulimwenguni.Kupitia mtandao huo alivujisha siri nzito sana za uwezo wa kivita wa marekani, silaha za kivita, tecknolojia, mbinu za kijeshi za marekani, oparesheni chafu za marekani. Katika historia ya ulinzi na usalama wa Marekani hajatokea mpuliza filimbi (whistle blower) aliyeweza kutoa siri nzito, za ndani zaidi na nyingi. Mwaka huo pekee Snowden alimpa mwandishi wa The Gurdian mafaili 10,000 ya siri. Pia njia nyingine aliyoitumia ni kufanya mahojiano na mwanahabaru sehemu ya siri na kisha kurushwa kwenye vyombo vya habari.
1481469175653.jpg

Snowden amekua akikutana na maafisa wa juu wa usalama wa nchi mbali mbali duniani kama Urusi, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Israeli na mshirika makubwa kama UN, World Bank, IMF na kuwaleza mipango ya Marekani kwa mataifa / mashirika hayo.

Kwasasa Snowden ni mmoja ya watu wanaoohitajika zaidi na Marekani, lakini ni ngumu kumdaka maana hata Mkurugenzi wa FBI James Comey aliwahi kusema... "Snowden akiwa CIA na NSA aliishi na magenius lakini wote kwake walikuwa ni taka taka". Unaambiwa Jamaa ana verified twitter account na huwa anarusha makombora mara chache chache.

LENGO/DHUMUNI KUU LA UZI HUU:

Mnamo mwaka 2011 serikali ya Marekani kupitia raisi wake Barack Obama ilithibitisha kwamba May 2 ya mwaka huo kikosi maalumu cha maangamizo kilifanikiwa kumtoa kwenye uso wa dunia adui namba 1 wa Marekani, Osama Bin Laden. Aliuwawa akiwa kwenye makazi yake Abboltabad, Pakistan kupitia oparesheni mkuki wa Neptune (Neptune spear) na mwili wake kuzamishwa baharini.

1481470557260.jpg
Daily mail waliandika kwenye kichwa cha habari "Kaoze kuzimu- Obama: Timu ya Wamarekani imemuua Osama kwenye pambano la moto"

May 2014, Snowden mpuliza filimbi, msaliti shujaa anaibuka kwenye mahojiano ya siri na kituo cha Moscow Tribune na kusema "The famous terrorist and former leader of Al-Qaeda is ALIVE and receives benefits from central intelligence Agency, CIA"-- "Gaidi maarufu na kiongozi wa Al-Qaeda yu hai  na anapokea fadhila kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA).
Alienda mbali na kudai kuwa taarifa za kifo cha Osama zilighushiwa ili kumuongezea sifa na mvuto wa kisiasa raisi Obama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2012. Snowden anaendelea "I have classified documents showing that Osama is still on CIA's payroll"-- "Nina document murua zinazoonesha kwamba Osama bado yupo kwenye malipo ya CIA".
"He still receives more than $100,000 a week which are being transferred through some front businesses and organisations directly to his Nassau bank account, I am not certain where he is now, but in 2013 he was living quietly in Bahamas in his Villa with his 5 wives and many children"-- "bado anapokea zaidi ya mil 209 tsh kwa week kutoka CIA, ambayo inahamishwa kibiashara na mashirika moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau. Sina uhakika alipo sasa, lakini mwaka 2013 alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana Bahamas yeye na wake zake wa5 pamoja na watoto wake wengi"
1481471638275.jpg

Snowden alidai kwamba "Osama bin Laden" ni mshirika (operative) mtiifu na makini wa CIA kwa muda mrefu sasa. Je tukio la Marekani kumuua Osama lingefikisha ujumbe gani kwa washirika pandikizi wa CIA? Kwamba nao wajiandae kuuwawa? Anaendelea kudadavua kwamba Marekani ilipanga shambuluo la bandia la kumuua Osama kushirikiana na Pakistan Secret service na hili tukio limemkumbatia Osama na kumfanya awe salama zaidi, kwasababu kila mtu ameamini Osama ameuwawa, hivyo hakuna mtu atakayejishughulisha kumsaka.

Leo hii Snowden akiwa na makosa yenye kifungo cha jumla ya miaka 120 yupo mafichoni katika nchi za Urusi na Brazil. Baadi ya watu wanamuona kama Msaliti wa usalama wa taifa na baadhi ya watu wanamuona ni mwananchi mzalendo. 1481472112843.jpg

UKWELI UNAOTHIBITISHA KUWA OSAMA HAKUUWAWA KWENYE OPARESHENI GERAMINO.

☆Kivipi Osama afe mara mbili, ni lini alifufuka?
Wachambuzi wa maswala ya kijasusi, viongozi wa nchi, wakuu wa taasisi za usalama waliwahi kuzungumza kwamba Osama alifariki miaka mingi iliyopita (2001). Afisa veterani wa CIA Robert Beir, kiongozi wa zamani wa FBI kitengo cha kupambana na ugaidi (counter - terrorism, waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Banazir Butto, Alex Jones wa CIA wote walidai Osama alifariki 2001. Katibu mkuu msaidizi wa Marekani Dr. Steve Pieczenik aliwahi kuthibitisha kwamba Osama alifariki kwa ugojwa wa 'Marfan Syndrome' na kwamba daktari wa CIA walifika kuupima mwili wa Osama akiwa hospitalini Dubai.

☆Mkanganyiko wa matukio ya oparesheni Geramino.
Kwanza tunaambiwa kulikuwa na majibizano ya risasi ya dakika 40, tena tunaambiwa hakukuwa na majibizano yoyote (kwamba mlinzi m1 wa Osama alitandikwa mkwaju akafariki na kisha kikosi cha FBI kikamfikia Osama.)
Tunaambiwa Osama alijeruhiwa vibaya, mara tena tunaambiwa Osama hakujeruhiwa bali alimtumia mkewe kama ngao.
Tunaambiwa makazi ya Osama yalikuwa ya ghali zaidi ya $1 million, ukweli ni kwamba kilikuwa ni kakibanda cha ovyo hata hakifiki robo ya hiyo pesa.
Taarifa alizotoa Obama na maafisa wa usalama na intelijensia zilikuwa zinapishana sana.

☆Kutupa mwili wa Osama baharini.
Baada ya watu kushambulia kitendo hicho, Obama aliibuka na kusema kwamba walifanya hivyo kufuata utaratibu wa Ibada ya mazishi ya kiislam. Lkn wanazuoni wa kiislam wakapinga vikali hoja hiyo wakidai kwamba muislam anaweza tu kuzikwa baharini endapo alifia baharini.

☆Uchunguzi wa sayansi wa vinasaba na sura.
Viongozi wa usalama walidai kwamba vipimo ya DNA na uchunguzi wa sura (facial recognition) vilifanyika ili kuhakiki pasi shaka kuwa mwili ule ulikua ni wa Bin Laden. Je ni kwanini vithibitisho hivi havijawahi kuwekwa popote hadharani?

☆Kughushi picha ya chumba cha matukio (situation room).
Ikulu ilitoa picha ikimuonesha rais Obama,Waziri wa mambo ya nnje H. Clinton, Makamu w rais Joe Biden na staff wengine wa ulinzi wakifuatilia shambulio lililomuuwa osama. Lakini baadae mkuu wa CIA, Leone Panette alikiri wazi kuwa Obama na team yake wasingeweza kushuhudia shambulio hilo 1 kwa 1 (live feed) kwani mitambo ya kurekodi tukio hilo ilizimwa ili isiingiliane na mawasiliano eneo la tukio.
Picha hii iliundwa mahsusi kumpa obama kiki ya kihistoria. 1481473938680.jpg

☆Tamko la Al-Qaeda.
Vyombo vya habari viliripoti kua Al-Qaeda wenyewe wamethibitisha kuuwawa kwa Osama. Lakini mchezo huu ulisukwa na shirika liitwalo SITE ambao ni mtandao maalumu wa kupika propaganda za shambulio la Pentagon. SITE ipo chini ya binti wa shushushu wa Israel mara kadhaa wamekuwa wakidakwa kutengeneza video kwa kutumia utaalamu wa juu kulingana na matakwa ya serikali.

☆Majirani wa mjengo wa Osama.
Majirani wa Osama ktk kijiji cha Abboltabad hawajawahi kuhisi tetesi zozote juu ya uwepo wa Osama hapo. Hata jeshi ya Pakistani ambalo lipo jirani walishindwa kung'amua uwepo wa Osama pia. Obama pia alithibitisha kua hawakuwa na uhakika 100% kuwa Osama alikuwa ndani ya lile jengo (ni kama kamari). Yawezekana aliuwa mtu tofauti kabisa na kuamua kuutangazia ulimwengua kuwa wamemuuwa osama ili kuficha aibu.

☆Osama alikuwa ni asset.
Asset katika dunia ya kiinteligensia ni kitu chochote chenye thamani/value ya kuweza kudukua taarifa muhimu. Inadaiwa gaidi aliyekamatwa porini ndiye aling'amua wapi Osama alipo baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa mateso (torturing interrogation) ndipo akafunguka. Iweje Osama ambaye alikuwa gaidi most wanted na biggest asset asikamatwe ahojiwe ili kung'amua taarifa za ugaidi wa ulimwenguni. Moja kwa moja aliuwawa wakati lengo la Marekani lilikuwa kumkamata akiwa hai (kwanini walimuuwa wakati kulikuwa na uwezekana wa kumkamata akiwa hai).
Swali la kujiuliza je ni kweli Osama alikua na ulinzi dhaifu kiasi kile? Ni kwanini marekani walifanya shambulio hili bila kuwashirikisha viongozi wa usalama wa Pakistan.

HITIMISHO:
Obama, ikulu ya marekani, taasisi na mashirika ya ujasusi ya Marekani na viongozi wa usalama wa Marekani hawajawahi kutoa tamko la kupinga/kukanusha filimbi aliyopuliza Bw. Snowden (Obama alijitahidi kujibu baadhi ya hoja za Snowden lakini kamwe suala la kifo cha Osama hajawahi kulizungumzia au  kukanusha).

Credit:Wikipedia-Daily Mail-Weakleaks-CNN-Mabalozi wa SHILAWADU.






Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.