Sunday, December 11, 2016

Ni kweli kuwa 'Hakkers' mitandaoni ndio chanzo cha Drake kusitisha kutoa album yake hadi mwaka 2017..?


Rapper Drake amesitisha mpango wake wa kuachia album yake mpya aliyoipa jina 'MORE LIFE' iliyotarajiwa kutoka Disemba 2016,ambapo sasa itaingia sokoni mwaka 2017.

Kupitia Sehemu ya vipindi vya 'OVOSOUND Radio' inayomilikiwa na Drake,Meneja wa rapper huyo mzaliwa wa Toronto,Canada Said El-Khatib alithibitisha uamuzi huo bila kuelezea sababu ya kuahirishwa kutoka kwa album hiyo.

 More Life is coming at the top of 2017,”.Alisema Khatib.


 Mwezi Oktoba mwaka huu,Drake kupitia OVOSOUND Radio,aliahidi ujio wa album mpya na kutaja baadhi  ya nyombo zilizomo kwenye album hiyo kama 'Two Birds', 'One Stone', ambazo zimetayarishwa na mtayarishaji maarufu wa miondoko ya 'Trap',London On Da Track pamoja na  'Sneakin' aliyowashirikisha 21 Savage na 'Fake Love'.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.