Saturday, December 17, 2016

Ujerumani kuzipiga faini Facebook,Twitter na Google kama hawatazivuta Habari za Kichochezi.


Serikali ya Ujerumani kupitia waziri wa Sheria Heiko Maas inatarajia kuwawekea vikwazo ikiwepo FAINI makampuni makubwa ya Mitandaoni Facebook,twitter na GOOGLE kama hawatafuta Hotuba za Chuki kwenye mitandao yao.

Serikali hiyo imewapa hadi masaa 24 yajayo wasipofuta habari hizo za chuki watapigwa fine isiyopunga TSH 1 Billion. Tayari kikosi maalumu cha facebook,twitter na GOOGLE kilikaa mwaka jana kushughulikia tatizo hilo lakini ripoti kutoka serikali ya Ujerumani inadai kuwa taarifa hizo nyingi hazijachukuliwa.


Heiko Maas,Waziri wa Sheria Ujerumani.





Tayari kwa Upande wa Facebook Hivi juzi wamezindua SOFTWARE maalum ya kugundua Taarifa Feki katika mtandao wake kabla haijarushwa.

Miongoni mwa taarifa zinazotajwa kuwa chanzo cha sakata hilo ni taarifa za kichochezi juu ya hatua ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na taarifa za uzushi juu kauli za viongozi wa Umoja huo juu ya ushindi wa Donald Trump kuwa rais wa Marekani,ushindi ambao uliwashangaza wengi ulimwenguni hasa kutokana na misimamo na kauli zake tata wakati wa kampeni.

Unaweza kusoma habari nzima kwa kubofya link hapa chini.

Germany to force Facebook, Google and Twitter to act on hate speech

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.