Kiungo wa Chealsea John Obi Mikel yupo mbioni kusitisha huduma ya kuitumikia klabu ya Chelsea kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari,akidaiwa kuwa kwenye mipango ya kwenda kucheza ligi kuu ya China ambapo zaidi ya klabu mbili zimeonesha kumtaka Mikel mwenye umri wa miaka 29.
Kiungo huyo raia wa Nigeria hajaonekana kwenye mchezo wowote msimu huu tangu kuwasili kwa kocha Antonio Conte ambae ameshindwa kumpa nafasi kwenye mfumo wake wa 3-4-3.
Taarifa imekuja wakati ambao Chelsea imetengeneza kiasi cha £52m. baada ya kumuuza kiungo wao Oscer kwenye klabu ya China inayofahamika kama Shangai SIPG.
Kiungo huyo alijiunga na The Blues mwaka 2006,akiwa amecheza michezo 374,akishinda mataji mawawili ya Ligi ya Uingereza,manne ya Kombe la FA na mawili ya Kombe la klabu Bingwa Ulaya.