Saturday, February 4, 2017

Mtoto Wa Jay Z Na Beyonce Kuzindua Bidhaa Hii




 Jay Z na mke wake Beyonce huenda wakawa ndio mastaa wanaoongelewa sana kwenye ulimwengu wa burudani  wiki hii baada ya Beyonce kuitangazia dunia kama ni mjamzito wa mapacha mapema.


Zikiwa hazijapita siku nyingi huku stori hiyo ikiendelea kuwa kubwa, tetesi zilizoufikia mtandao wa TMZ ni ishu ya Mtoto Blue Ivy Carter kuzindua bidhaa yake ambayo athusika zaidi kwenye vipodozi vya nwyele ikifuatiwa na ufunguzi wa saloon yake.


Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ inasemekana kampuni ya Beyonce ipo kwenye hatua za mwisho kabisa za uzinduzi wa brand hiyo mpya itakayojulikana kama “Blue Ivy Carter” ukiachana na mambo za urembo pia bidhaa hiyo ya "Blue Ivy Carter" itakuja na nguo za umeme pamoja na games za watoto.


Huu ulikua ni mpango wa kitambo ambao ulipangwa kufanyika mapema mwaka 2012 lakini ulishindikana baada ya Jay Z na Beyonce kushindwa kupata usajil kufuatia kuwepo na kampuni iliyokua ikitumia jina la "Blue Ivy" hivyo wameamua kuongeza neno "Carter" kitendo ambacho kitamfanya mtoto 'Blue Ivy" kumiliki Brand yake akiwa na umri wa miaka 5 tu.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.