Kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa uwepo kwa baadhi ya alama kwenye miili yao huwa na maana kwenye maisha yao.Inaweza kuwa bahati,nuksi au pengine huwakilisha tabia ya tofauti kwenye mwili wa mtu husika.
Hizi ni baadhi tu ya maana ya alama hizo,ila ikumbukwe kuwa alama hizi ni zile za kuzaliwa na sio makovu.
ALAMA NA MAANA ZAKE.
Mguuni,mkononi au kwenye vidole -Kwa wachina alama kwenye mwili inawaweza kuwa bahati au nuksi ila inategemea ina rangi gani na ipo sehemu gani,kwa mfano alama yenye rangi nyeusi ikiwa mguuni inaelezea mhusika ni mtu wa kusafiri,inaweza pia kuwa alama yenye rangi ya "dark red" rangi ya damu ya mzee kama wengi wanavyoiita na ikiwa ipo mkononi humanisha kuwa mhusika ana ujuzi fulani au jambo fulani linalohusu mkono huo.
Mwanamuziki Vanessa Mdee.
Karibu na Pua -Inadawa alama inapokuwa kwenye eneo la uso humaanisha mambo mazuri ila inategemea alama ipo eneo gani,watu hawa wengi huwa maarufu,wenye ujuzi wa tofauti ila pia ikiwa karibu na pua humanisha mhusika sio mtu wa kukasirika mapema.Pia baadhi yao huwa na sifa ya kuwa viongozi.
Jaji na waziri mkuu mstaafu,Joseph Sinde Warioba.
Mdomoni - hapa humanisha mhusika kuwa na maisha ya wastani,mafanikio,umaarufu ila pia kwa upande wa wanaume humaanisha mhusika ni mtu wa kupenda wanawake.
Mwigizaji Angelina Jolie.
Kichwani - Hapa humaanisha mhusika amejaliwa madaraka katika mambo fulani,wengi wao huwa wanasiasa au wanaharakati.Pia hupenda mijadala na kujishuhulisha hata kwenye mambo yasiyowahusu.
Kwenye jicho kulia au kushoto - Humaanisha mhusika kuwa mtu wa bahati na fedha,anaweza asiwe mtafutaji ila ni mtu mwenye bahati.Kwa upande wa wanaume alama ikiwa pembezoni mwa jicho humaanisha mhusika ni mtu wa kupenda wanawake na ni msiri sana,jambo linalomuhusu hawezi kuongea mbele za watu,mara nyingi huwa kimya na hawapendi kuzungumza maana muda mwingi wanautumia kuwaza mambo yao.Ila sio watu wenye kupenda ugomvi lakini pia alama ikiwa chini ya jicho humanisha upendo au upole.
Mwanamitindo,Jokate Mwongelo.
Kwenye sikio,shingoni au nyuma ya kichwa - Hapa humaanisha mhusika ni mtu wa kujiheshimu na mwenye mipango,huwezi kumdanganya kirahisi kwa kuwa hufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi.
Rapper na mfanyabiashara,P-Diddy.
Kwenye ulimi - Hapa humanisha mhusika kuwa tatizo la kiafya japo linaweza lisionekane mapema,wengi wao huwa wazungumzaji na wenye umakini sana.Pia wanapenda kula,kucheza na kuongea na watoto ila pia ni watu wenye maono.
Raisi Barack Obama.
Kwenye bega au mgongoni - Hapa humanisha mhusika kuwa mtu wa kupenda marafiki,ni watu wenye hisia na ni rahisi kuwa rafiki wa mtu yeyote.
Rapper,Nas Escobar.
Puani - Ni maajabu ila inadaiwa alama inapokua puani humanisha nukisi au jambo baya kwenye maisha ya mhusika.Mara nyingi ni watu wa kupenda starehe,wenye hasira ila pia huandamwa na changamoto nyingi kwenye maisha yao.
Je unafikiri mitazamo hii ina ukweli ndani yake...??
Showing posts with label Makala. Show all posts
Showing posts with label Makala. Show all posts
Thursday, September 8, 2016
Tuesday, September 6, 2016
Wachunguze wanawake wanaopenda nyimbo hizi kabla ya ku-date nao.
Ikiwa unahitaji mahusiano ya kudumu na mwanamke mmoja huna budi kujiepusha na wanawake wa aina hii.
Anaenda maisha ya starehe.
Unakutana na mwanamke ambae kila siku ya weekend yuko katika klabu za usiku na huwa na rafiki zake wa kike wakinywa pombe, wakivuta bangi, shisha
au sigara na wala huoni muda analipa bili then unaona picha zake akiwa na
rafiki zake na ukiangalia kwa makini utamwona akiwa na marafiki tofauti
wa kike na kiume katika kila picha kwenye mitandao yake ya kijamii,basi jua huyo siyo mtu mwenye malengo au mipango ya muda mrefu.
Uhusiano wa karibu na wanaume tofauti.
Mwanamke wa aina hii mara nyingi anaweza kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume tofauti kwa wakati mmoja.Kazi yake kubwa ni
kujisifu kwa wenzie kuhusu mahusiano yake na wanaume hao ambao yuko nao
na kuchat nao kwenye simu wakati wote. Sio muda wote ataweza kujibu text zako au kupokea simu zako kwa wakati na atakupa
visingizio vingi tu, yule rafiki yangu tu, yule nafanya nae kazi, yule
tumekuwa wote mtaani.Kuna wakati inaweza kuwa kweli lakini lazima kuna mtu
katika hao aliokupa maelezo yake ambaye tayari ameshakuwa nae,yuko
nae,au ana mipango ya kuwa nae kimapenzi.
Hujitongozesha/Hujilengesha.
Na kwa tabia hii, hujikuta yuko kwenye
mahusiano na mwanamume aliye na familia ama mwenye mchumba anayetaka
kumuoa.Pia haokupi kutoka kimapenzi na mume wa rafiki yake au dada yake.
Hizi ni baadhi ya nyimbo zinazopendwa na Wanawake wa aina hii :
Freak like me – Adina Howard
I’m a survivor- Destiny’s Child
Miss Independent – Neyo
Irreplaceable- Beyonce
Single Ladies- Beyonce
Girl on Fire- Alicia Keya
No scrubs- TLC
I’m every woman- Chaka Khan
Binadamu tumetofautiana sura mpaka tabia,hivyo tunaposema wanawake hatuamanishi wote bali baadhi yao.
Monday, September 5, 2016
Mambo 10 ya kujua kuhusu upandikizi wa makalio feki.
Miongoni mwa tamaduni hizo ni pamoja na upandikizaji wa makalio bandia ambao umekua maarufu hata hapa Tanzania,hivyo basi haya ni mambo 10 muhimu kuhusu upandikizaji wa makalio bandia kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa masuala ya afya wa unaofahamika kama https://www.realself.com/Butt-implants/reviews
1.Unaweza kupata maumivu makali sana - Ila inategemea na njia gani ya uongezaji unayoitumia,unaweza kushindwa kukaa kwa muda wa wiki tatu,namaanisha mwezi mmoja kasoro wiki moja.
Mwanamitindo Amber Rose,ni miongoni mwa watu maarufu wanaotajwa kupandikiza makalio bandia.
3.Mabadiliko huanza kuonekana baada ya masaa 120 - Haijalishi utatumia njia ya upasuaji au sindano hivyo endapo matokeo ya dawa kufanya kazi yatazidi siku tano (masaa 120),basi jua umetapeliwa.
4.Mabadiliiko hayategemei unene au wembamba wa mtu - Watu wengi wamekua wakidhani kuwa Wanawake wanene ndio wenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kwenye zoezi hili la kupandikiza makalio bandia,ila ukweli ni kwamba kinachokuzwa ni makalio hivyo unaweza kuwa mwembamba na makalio yako yakaonekana makubwa kwakua dawa nyingi zimetengenezwa maalum kwa kusisimua misuli ya eneo husika,japo baadhi ya watu hupata madhara na dawa kufanya kazi kwenye maeneo mengine ya mwili ambayo hayakukusudiwa.
Mwanamitindo na modal,Blac Chyna nae yumo kweli list ya mastaa waliopandikiza makalio bandia.
5.Ni uamuzi wako kudungwa au kutodungwa sindano ya ganzi wakati wa upandikizi - Madaktari wenye uzoefu na zoezi hili hupendekeza mteja apewe dawa ya kuzuia maumivu wakati wa upandikizi,upandikizi wa aina hii kitaalam hufahamika kama "general anesthesia",ingwa bei yake ni tofauti na upandikizi wa kawaida bila ganzi,"local anesthesia".
6.Utamaduni wa kupandikiza makalio umezidi kuwa maarufu ulimwenguni - Achila mbali kuwa watu maarufu waliopandikiza makalio wamekua chachu ya wanawake wengi kutamani maumbo ambayo hawakuzaliwa nayo,idadi ya wanawake wanaofanya upasuaji wa kuongeza makalio imekua ikiongezeka siku hadi siku kwani kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO),zaidi ya wanawake 12,000 walifanyiwa upasuaji ili kukuza makalio yao huku idadi hii ikiwa ni mara mbili ya idadi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji wa aina hiyo mwaka 2013.Hata hivyo takwimu hizi zililenga zaidi wanawake ambao walifanyiwa upandikizi kitaalam na madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa aina hiyo.
7.Hata wanaume hufanya upandikizi wa makalio pia - Unaweza usiamini ila kwenye mataifa ya magharibi hili sio jambo la kushangaza.
Mwanamitindo,Kim Kardashian
9.Gharama za upandikizi kwa njia ya mkato ni rahisi zaidi - Wanawake wengi wamekua wakibadili maumbo yao kwa njia zisizo rasmi au kwa kuwatumia wataalam wasio na taaluma ya zoezi hili kwakua bei huwa rahisi.Kwenye nchi kama Marekani upasuaji wa njia za mkato hugharimu kati ya $100 hadi $200.
10.Inadaiwa wanaume ndi chanzo cha wanawake wengi kutaka kubadili maumbo yao - Tafiti zinaonesha kuwa wanawake wenye makalio makubwa huwa kwenye wakati mgumu sana kwani hutongozwa na wanaume wengi,hii ikimaanisha kuwa wanaume wengi hupenda wanawake wenye makalio makubwa hivyo pengine hii ndo sababu ya wanawake wengi kupandikiza makalio bandia.Na kwa kuthibitisha hili hata hapa bongo mwanamke mwenye makalio makubwa anapopita barabarani wanaume wakware huwaishi kumtazama au kumjadili,si ajabu hata dereva wa gari akashusha kioo ili kusafisha macho.
MY TAKE :
Sidhani kama ni jambo la busara kufata mkumbo kwa kutafuta uzuri ambao baada ya muda utakusababishia matatizo,njia sahihi ni kufanya mazoezi na kula mlo kamili.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
facebook

















