Monday, September 5, 2016

Mambo 10 ya kujua kuhusu upandikizi wa makalio feki.

Ni wazi kuwa utandawazi umekua na matokeo chanya kwenye maisha yetu hasa katika ulimwengu huu ambao dunia imegeuka kuwa kijiji,ila pia utandawazi umekuja na aina nyingine za tamaduni ambazo raia waliopo kwenye nchi zinazoendelea wamekua wakiiga tamaduni hizo ambazo nyingine  huwa na matokeo hasi au madhara kwa ujumla.

Miongoni mwa tamaduni hizo ni pamoja na upandikizaji wa makalio bandia ambao umekua maarufu hata hapa Tanzania,hivyo basi haya ni mambo 10 muhimu kuhusu upandikizaji wa makalio bandia kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na  mtandao wa masuala ya afya wa unaofahamika kama https://www.realself.com/Butt-implants/reviews


1.Unaweza kupata maumivu makali sana - Ila inategemea na njia gani ya uongezaji unayoitumia,unaweza kushindwa kukaa kwa muda wa wiki tatu,namaanisha mwezi mmoja kasoro wiki moja.

 2.Kuna uwezekano uongezaji ukashindikana - Kwa wale wanaotumia njia ya sindano ambapo hudungwa mchanganyiko wa dawa za kusisimua misuli,baada ya muda wanaweza kupoteza maumbo yao mapya wanayotaka kutokana na maungo husika kulegea au kupata madhara zaidi.Tatizo hili hutegemea damu ya mtu na aina ya mchanganyiko wa dawa.
 Mwanamitindo Amber Rose,ni miongoni mwa watu maarufu wanaotajwa kupandikiza makalio bandia.

 3.Mabadiliko huanza kuonekana baada ya masaa 120 - Haijalishi utatumia njia ya upasuaji au sindano hivyo endapo  matokeo ya dawa kufanya kazi yatazidi siku tano (masaa 120),basi jua umetapeliwa.

4.Mabadiliiko hayategemei unene au wembamba wa mtu - Watu wengi wamekua wakidhani kuwa Wanawake wanene ndio wenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kwenye zoezi hili la kupandikiza makalio bandia,ila ukweli ni kwamba kinachokuzwa ni makalio hivyo unaweza kuwa mwembamba na makalio yako yakaonekana makubwa kwakua dawa nyingi zimetengenezwa maalum kwa kusisimua misuli ya eneo husika,japo baadhi ya watu hupata madhara na dawa kufanya kazi kwenye maeneo mengine ya mwili ambayo hayakukusudiwa.
  Mwanamitindo na modal,Blac Chyna nae yumo kweli list ya mastaa waliopandikiza makalio bandia.

5.Ni uamuzi wako kudungwa au kutodungwa sindano ya ganzi wakati wa upandikizi - Madaktari wenye uzoefu na zoezi hili  hupendekeza mteja apewe dawa ya kuzuia maumivu wakati wa upandikizi,upandikizi wa aina hii kitaalam hufahamika kama "general anesthesia",ingwa bei yake ni tofauti na upandikizi wa kawaida bila ganzi,"local anesthesia".
 6.Utamaduni wa kupandikiza makalio umezidi kuwa maarufu ulimwenguni - Achila mbali kuwa watu maarufu waliopandikiza makalio wamekua chachu ya wanawake wengi kutamani maumbo ambayo hawakuzaliwa nayo,idadi ya wanawake  wanaofanya upasuaji wa kuongeza makalio imekua ikiongezeka siku hadi siku kwani kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO),zaidi ya wanawake 12,000 walifanyiwa upasuaji ili kukuza makalio yao huku idadi hii ikiwa ni mara mbili ya idadi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji wa aina hiyo mwaka 2013.Hata hivyo takwimu hizi zililenga zaidi wanawake ambao walifanyiwa upandikizi kitaalam na madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa aina hiyo.

7.Hata wanaume hufanya upandikizi wa makalio pia - Unaweza usiamini ila kwenye mataifa ya magharibi hili sio jambo la kushangaza.
8.Madhara ya kupandikiza makalio feki hayakwepeki - Madaktari wanadai kuwa,upandikizi wa makalio bandia huambatana na madhara ya kiafya,mwanzoni unaweza kuwa sawa na ukafikiri kuwa lengo lako limefanikiwa ila kwa wastani baada ya miaka 10 mwili huchoka na na kupelekea mhusika kupata matatizo ya kiafya kama,kupooza,majipu,upele,makalio kulegea nk.
                                              Mwanamitindo,Kim Kardashian


 9.Gharama za upandikizi kwa njia ya mkato ni rahisi zaidi - Wanawake wengi wamekua wakibadili maumbo yao kwa njia zisizo rasmi au kwa  kuwatumia wataalam wasio na taaluma ya zoezi hili kwakua bei huwa rahisi.Kwenye nchi kama Marekani upasuaji wa njia za mkato hugharimu kati ya $100 hadi $200.

        Mwanamuziki Nick Minaj ni miongoni watu maarufu wanaodaiwa kupandikiza makalio bandia.

10.Inadaiwa wanaume ndi chanzo cha wanawake wengi kutaka kubadili maumbo yao - Tafiti zinaonesha kuwa wanawake  wenye makalio makubwa huwa kwenye wakati mgumu sana kwani hutongozwa na wanaume wengi,hii ikimaanisha kuwa wanaume wengi hupenda wanawake wenye makalio makubwa hivyo pengine hii ndo sababu ya wanawake wengi kupandikiza makalio bandia.Na kwa kuthibitisha hili hata hapa bongo mwanamke mwenye makalio makubwa anapopita barabarani wanaume wakware huwaishi kumtazama au kumjadili,si ajabu hata dereva wa gari akashusha kioo ili kusafisha macho.

MY TAKE :
Sidhani kama ni jambo la busara kufata mkumbo kwa kutafuta uzuri ambao baada ya muda utakusababishia matatizo,njia sahihi ni kufanya mazoezi na kula mlo kamili.



Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.