Showing posts with label Tetemeko la ardhi Kagera. Show all posts
Showing posts with label Tetemeko la ardhi Kagera. Show all posts
Wednesday, November 16, 2016
Kizungumkuti cha fedha za misaada kwa waathirika wa tetemeko kutafunwa;Serikali yatoa ufafanuzi.
Baada ya mijadala mingi kuhusu michango kwa waathirika wa tetemeko mkoani Kagera, serikali imetoa ufafanuzi kuhusu michango hiyo.
Serikali imesema imeshapokea misaada ya Vifaa, Chakula, Fedha na ahadi zenye thamani ya Sh. bilioni 15.19 kwa ajili ya Wahanga wa Tetemeko mkoani Kagera.
Zinahitajika jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 104.9 kwa ajili ya kukabiliana na maafa ya tetemeko ili kuurudisha mkoa huo katika hali yake halisi.
Pia imesema kuwa baadhi ya nchi zilizotoa ahadi kama Serikali ya Uingereza, wameahidi kutekeleza ahadi hiyo kwa kujikita moja kwa moja katika ujenzi wa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo.
Friday, September 23, 2016
PICHA 5:Mh.Lowassa alipowatembelea wahanga wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,Edward Lowassa leo aliwasili mkoani Kagera na kuwafariji wahanga wa tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10 mwaka huu na kusambabisha vifo vya watu 19 huku zaidi ya 250 wakiachwa na majeraha mbalimbali.
Katika ziara hiyo Mh.Lowassa aliongozana na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema,Shekh Katimba,Khamis Mgeja na Mbunge wa Bukoba Mjini,Wilfried Lwakatare.
Katika ziara hiyo Mh.Lowassa aliongozana na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema,Shekh Katimba,Khamis Mgeja na Mbunge wa Bukoba Mjini,Wilfried Lwakatare.
Mh.Lowassa akiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jererali mstaafu Salim Kijuu.
Thursday, September 15, 2016
Matembezi ya hisani kwa wahanga wa tetemeko Sept.17.
Matembezi hayo yaliyopewa jina la ‘Walk For Kagera’ yatafanyika
Jumamosi, September 17. Yatafanyika kuanzia Police Officer’s Mess saa
saa 12 asubuhi, huku ada ya ushiriki ikiwa ni shilingi 10,000 za kitanzania.
Matembezi hayo ya hisani yameandaliwa na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ikishirikiana na ofisi ya waziri mkuu,ambapo lengo kuu la matembezi hayo likiwa ni kuchangisha fedha za kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
facebook