Matembezi hayo yaliyopewa jina la ‘Walk For Kagera’ yatafanyika
Jumamosi, September 17. Yatafanyika kuanzia Police Officer’s Mess saa
saa 12 asubuhi, huku ada ya ushiriki ikiwa ni shilingi 10,000 za kitanzania.
Matembezi hayo ya hisani yameandaliwa na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ikishirikiana
na ofisi ya waziri mkuu,ambapo lengo kuu la matembezi hayo likiwa ni kuchangisha fedha
za kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.