Na Mwaija Salum
STAA wa songi la Money Money, Hamis
Kinzasa ’20 Percent’ amemwagana na mkewe ambaye ni msanii mwenziye,
Whitney John, baada ya kutofautiana sera.
Chanzo makini kilichoomba
hifadhi ya jina kimesema, staa huyo amefikia hatua ya kumwagana na mzazi
mwenziye huyo waliyeishi naye kwa muda mrefu kutokana na kuwajali zaidi
marafiki kuliko mkewe huyo.
“Mkewe ameamua kurudi nyumbani kwao
Ubungo jijini Dar baada ya kuona jamaa haeleweki, anawajali zaidi
marafiki zake kuliko familia,” kilisema chanzo hicho.
Whitney alipotafutwa na paparazi wetu, alikiri kurudi nyumbani kwao Ubungo na kushusha lawama zake:
“Tangu
aliposhinda zile tuzo tano alikuwa akipata sana shoo, nilikuwa
nikimwambia tupange mambo ya kimaendeleo lakini hakusikiliza, kutwa
akawa anakwenda Morogoro kwa Afande Sele akiishiwa hela ndiyo anarudi
Dar.
“Licha ya kuwa nimezaa naye na kuishi naye kwa muda mrefu na kumvumilia sana nimeamua kuachia ngazi,’’ alisema Whitney.
Alipotafutwa 20 Percent kwa njia ya simu, hakupatikana hewani. Jitihada za kumtafuta bado zinaendelea!
Thursday, May 2, 2013
Comments System
facebook