Thursday, May 2, 2013
20 PERCENT, MZAZI MWENZAKE WAMWAGANA
Na Mwaija Salum wa Global Publisherstz
STAA wa songi la Money Money, Hamis Kinzasa ’20 Percent’ amemwagana na mkewe ambaye ni msanii mwenziye, Whitney John, baada ya kutofautiana sera.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kimesema, staa huyo amefikia hatua ya kumwagana na mzazi mwenziye huyo waliyeishi naye kwa muda mrefu kutokana na kuwajali zaidi marafiki kuliko mkewe huyo.
“Mkewe ameamua kurudi nyumbani kwao Ubungo jijini Dar baada ya kuona jamaa haeleweki, anawajali zaidi marafiki zake kuliko familia,” kilisema chanzo hicho.
Whitney alipotafutwa na paparazi wetu, alikiri kurudi nyumbani kwao Ubungo na kushusha lawama zake:
“Tangu aliposhinda zile tuzo tano alikuwa akipata sana shoo, nilikuwa nikimwambia tupange mambo ya kimaendeleo lakini hakusikiliza, kutwa akawa anakwenda Morogoro kwa Afande Sele akiishiwa hela ndiyo anarudi Dar.
“Licha ya kuwa nimezaa naye na kuishi naye kwa muda mrefu na kumvumilia sana nimeamua kuachia ngazi,’’ alisema Whitney.
Alipotafutwa 20 Percent kwa njia ya simu, hakupatikana hewani. Jitihada za kumtafuta bado zinaendelea!
Comments System
facebook