Katika ile Scandal inayomkabili Msanii wa Bongo Flava (Ally Ramadhani) maarufu kama A.T akituhumiwa na Mganga wa Kienyeji aliyejitambulisha kwa jina la Sharif, kwamba eti hakumlipia pango la nyumba kama Ujira wake baada ya Mganga huyo kumfanyia matibabu ya kijadi msanii huyo, Mganga wa Kienyeji ameamua kwenda kumpeleka A.T kwa pilato (Mahakamani)
Gazeti la Makorokocho limefanikiwa kuchungulia
barua ya A.T kuitwa mahakamani na atatakiwa kuongozana na mashahidi iwapo
atashindwa kutokea mahakamani bila taarifa basi Hakimu atatoa ushindi kwa mdai
ambaye ni Mganga wa Kienyeji anayedai alipwe milioni 3 kama Bill ya matibabu
aliyompa AT, ikiwemo na kumsafisha Nyota na kusababisha msanii huyo kushinda
Tuzo moja katika Kili Tanzania Music Awards.