|
Maneck |
Mtaarishaji wa Muziki katika Studio za A.M Records Tandale Maneck amevunja ukimya baada ya kushutumiwa na Msanii Ommy Dimpoz kuwa eti amevujisha Wimbo wa Dimpoz bila kuwepo makubaliano kati yao, na Dimpoz alitiririka kuwa ngoma hiyo aliierecord mwaka juzi pale A.M Records yeye akaondoka na Rough Copy ikiwa haijamaliziwa, lakini akashangaa hivi karibuni anaiona ngoma hiyo mtaani ikiwa imekamilika kila kitu Sound Nzuri tofauti na mwanzo kwa hiyo lazima Studio ndo wamevujisha,
sasa wakati akijibu shutuma hizo mmoja kati ya wamiliki wa Studio hiyo Maneck amesema sio kweli wao wamevujisha, na kuna wasanii anawajua hawataji majina yao kuwa eto ndio zao kujaribu soko mtaani kwa kuvujisha nyimbo zao na ikikubali ndo wanazi release Radio,
Maneck akaongeza kwa kusema mbona yeye ana kazi za wasanii kibao Studio kama The Late Albet Mangwea Album Nzima, Quick Rocka na wengine, lakini Mbona hazivuji? akamalizia kwa kuhoji...