Wednesday, February 12, 2014

U HEARD : SHILOLE KATI KATI YA PENZI LA MADEE NA NUH MZIWANDA (INASEMEKANA LAKINI)



Inasemekana Eti Msanii wa Bongo Flava ambaye pia ni Muigizaji wa Bongo Movie Mwanadada Shilole kwa wakati huu yuko katika mahaba mazito na Up Coming Artist Nuh Mziwanda lakini kabla ya kuwa na Nuh Eti alikua anatoka na msanii mkongwe wa Bongo Flava Madee,

Madee
Sasa utata umeibuka baada ya Shilole Kuandaa Show Kijijini Kwao Igunga Tabora akawa ameamua kuwachukua Nuh na Madee pamoja  Queen Darlin waende kushambulia Jukwaa la Igunga, hadi matangazo yalikua yameshatengenezwa lakini kumbe Madee alikua Hajui kama katika Show Hiyo Nuh ataenda, taarifa zilizofika mezani kwa muhariri zinadai kuwa eti Madee aliposhtukia mchongo kuwa Nuh pia anaenda, ikabidi amshtue meneja wake ambaye ni Babu Tale awaambie kina Shilole kuwa kama Nuh Mziwanda ataperform katika Show hiyo basi yeye Madee haendi Igunga,

Nuh Mziwanda
Ujumbe ulipomfikia Shilole akapima uzito wa wasanii hao mwisho wa siku akaona poa Bora Nuh abaki Dar kwa sababu hana nguvu ya kuvuta mashabiki wakati Madee ana uhakika akiwepo basi watu kibao watajitokeza, Show ya Shilole Mkoani Tabora inatarajiwa kufanyika Weekend hii inayokuja ya Valentine, inasemekana Lakini

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.