|
Didas Facion wa Turabi akiwa Ubalozi wa Tanzania |
Mwaka Jana Mwanadada ambaye ni Promota Mkongwe wa Muziki wa kizazi Kipya nchini Uingereza Mzalendo wa Ki Tanzania Didas Facion alienda Mile nyingi zaidi mbele kwa Kuanzisha Didas Entertainment ikiwemo Internet Radio & TV, sherehe za uzinduzi huu wa ki V.I.P zilifanyika Milton Kiln Farm Pub, Milton Keynes United Kingdom sherehe ambazo zilihudhuriwa na watu wengi, uzinduzi huo ulienda sambamba na uzinduzi wa Webisite ya www.didasentertainment.com Pongezi nyingi kwake na kwa Team yake pia, manake kama sikosei karibu miaka miwili iliyopita Didas alianza na radio ya mtandaoni nakumbuka kuskiza baadhi ya Vipindi kupitia mitandao mingine, lakini kutokana na ujio wa Website yake bila shaka vipindi sasa vitaanza kuruka humo, lakini ongezeko la Tv pia litarahisisha wasanii Wa Bongo Flava na waburudishaji watakaotembelea U.K wataonekana humo, mpango mzima wa Uzinduzi cheki video hapo chini uone ilivyokua siku hiyo