|
Fid Q akikabidhiwa Tuzo na Adam Mchomvu |
Mshindi wa Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop na Mwandishi bora wa mashairi ya hiphop (KTMA 2014) Rapper Fid Q baada ya kuchukua tuzo hizo amesema mpango wake ni kufundisha wasanii jinsi ya kufanya Hiphop inayoweza kufanya vizuri kwenye vituo vya radio kwa sababu kwa wakati Tanzania Hiphop haifanyi vizuri Radio, Fid amesema amesubiri tuzo hizo kwa miaka saba kwani mara ya mwisho kuchukua tuzo ni mwaka 2007 Ni Hayo tu kama wimbo bora wa hiphop na mwaka 2006 alipata Tuzo kupitia wimbo wake wa Mwanza Mwanza, na Mwaka 2011 alipata tuzo kupitia category ya Wimbo Bora wa Kushirikiana wa JCB na mwaka huu tuzo zimerudi nyumbani, FiD Q ameongeza kuwa ameshinda kwasababu anastahili na kama asingepata basi tuzo zisingekua za ukweli kwasababu watu kitaani wameridhika na matokea ya mwaka huu katika Kili Tanzania Music Awards, Fid Q anasema ushindi wake umewafurahisha watu wengi sana, viongozi serikalini wamekua wakimpigia simu kumpongeza, masela wa kitaa, masista duu na mabrazameni.