Msanii wa Bongo flava kipengele cha Hiphop Nash Mc amedaiwa kumpachika Kibendi Mwanadada mmoja anayefahamika kwa jina Subira, kwa mujibu Subira anadai kuwa alikua katika mahusiano ya Kimahaba na Rapper Nash Mc kwa muda wa takribani miezi sita, ndani ya kipindi hiko ndio akaanza kujiskia kichefuchefu kizunguzungu akamwambia aliyekua Boy Friend wake Nash Mc na wakakubaliana kuwa Subira akanunue kipimo kidogo cha ujauzito katika Pharmacy ya jirani na kwao enzi hizo akiishi Temeke, alipoenda kujipima nyumbani akakuta hamna kitu, lakini siku zinavyoenda Mwanadada akawa anaona chenga chenga ikabidi aende hospitali kupima na matokeo yakaja kuwa ana ujauzito, Subira anadai kuwa alipomtaarifu Nash Mc jamaa akaruka futi mia tisa tisini na tisa kuwa hausiki, taarifa zikafika kwa wazazi walezi wa Subira ambao alikua anaishi nao, wakamwitisha Nash Mc lakini msanii huyo eti alikataa kufika mpaka leo, sasa walezi wa binti wakamfukuza Subira na sasa hivi anaishi morogoro, Subira ameyaongea haya kwa masikitiko huku analia, na amedai kuwa Mimba yake kwa wakati huu imefikisha miezi mi tano,
Gazeti la Makorokocho linaendelea kumtafuta Nash Mc mwanzo nilimpigia akadai kuwa hawezi kuongelea ishu hiyo kwa sababu yuko ofisini kwa hiyo nitamfute baadae, Taarifa hizi bado hazina Uhakika mpaka Nash Mc atakapothibitisha au vipimo vya DNA vikifanyika.
Sikiliza Sauti ya Subira Akitiririka na Gossip Cop kama ilivyokua leo kwenye XXL