Linex amelalamikiwa na m'bunifu wa Nembo za Tshirt aliyejitambulisha kwa jina la James Samwel mkazi wa Kawe jijini Dar es salaam, amedai kuwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita alikutana na Linex na kumwonyesha T Shirt zenye chata ya Kimugina akamwomba msanii huyo akatangaze ili watu wakihitaji kununua wawe wanagawana na pesa (Linex na James) sasa James anadai siku ya tukio Linex alifurahia tshirt hizo na kuivaa moja hapo hapo na wakaachana, lakini siku zilizofata eti Linex akampigia simu james na kumwambia anahitaji tshirt nyingine mbili kwa ahadi kuwa atamlipa elfu 15 kwa kila moja, James anadai tangu siku hiyo eti Linex anamzungusha sana pesa yake hamlipi kwa hivyo yeye anachotaka ni mtonyo wake tu na siku kitu kingine, akizungumzia Scandal hili Linex amejibu kuwa yeye hawezi kumlipa Dogo pesa kwasababu dogo amekua akiuza kupitia mgongo wa Linex kwani Neno "Kimugina" ni jina la wimbo wake
James Samwel mchizi anayedai kutapeliwa na Linex |