Friday, July 18, 2014

BABA LEVO AUNGANA NA MTOTO WAKE BAADA YA KUMPIGANIA KWA MIAKA 9

Baba Levo akiwa na Mtoto wake Revocatus
Miaka Tisa iliyopita Msanii wa Bongo Flava Clayton Revocatus a.k.a Baba Levo wakati huo akiwa na umri wa miaka 19 mkoani Kigoma alitengana na Binti waliyekua wakiishi nae pika pakua kwa muda wa miaka miwili, Binti akapata mimba ya Baba Levo na mwaka huo huo mwanadada akajifungua mtoto wa kiume waliyekuja kumwita Revocatus hapo ndipo Msanii huyu akajiita Baba Levo (Yaani Baba Revocatus) baada ya muda mfupi Binti akaolewa na Jamaa mwingine kuona Hivyo Baba Levo akaomba apewe mtoto amlee mwenyewe Mama mtoto akakataa ikabidi suala liende hadi ustawi wa jamii, shauri likaendeshwa lakini kwa bahati mbaya Baba Levo akaishindwa kesi na kuamuriwa aendelee kutoa huduma kwa ajili ya malezi ya mtoto wake, miaka ikawa inapita mpaka Juzi alipopigiwa simu na mzazi mwenzake na kuambiwa kama bado ana nia ya kumchukua mtoto wake basi atume nauli ya mtoto ili aje Dar es salaam, Baba Levo fasta akatuma nauli hiyo na mtoto wake akaingia jijini Jana Usiku akitokea Shinyanga ambako alikua akiishi na Mama yake pamoja na baba wa Kambo.
Of Course Baba Levo kwasababu bado ni bachelor basi anajiunga kwenye orodha ya wasanii wenye watoto na wanawalea wenyewe kama Fid Q.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.