Saturday, July 5, 2014

RAY C NA TID NI WAARABU WA PEMBA (UGOMVI WAO USIINGILIE)

Kutoka Kushoto ni TID, Ray C na Q Chila ambaye naye aliwahi kujitangaza kuwahi kutumia madawa ya Kulevya na kuacha
Story Kubwa wiki hii ilikua inamhusu TID dhidi ya Ray C Msanii wa Bongo flava aliyewahi kujitangaza kuwahi kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroine na Cocaine yaliyomrudisha nyuma kimaendeleo kwa miaka kadhaa hadi kufikia hadhi ya uzururaji na baadae akaja kusaidiwa na Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete kwa kusaidiwa gharama za matibabu ya kuacha madawa hayo, baadae mwaka huu Ray C akaanzisha harakati za kuwasaidi wateja wengine mtaani wakiwemo watu maarufu wanaotumia madawa hayo, zaidi ya wiki moja iliyopita alijikuta akikwaa kisiki na kuambulia matusi ya nguoni kutoka kwa msanii mwenzake wa Bongo Flava Khalid Mohammed a.k.a TID
Inasemekana Ray C ali coment kwenye Post ya TID Instagram kwa kumwambia msanii huyo amtafute, kauli ambayo Tid aliichukulia tofauti na kuanza kumshushia maneno mazito
Kwa mujibu wa TID anasema kama kweli Ray C alikua ana shida na yeye kwanini amwandikie kwenye Mitandao? kama anataka kulala naye yeye TID hatakiiii kwani Ray C ni Bad Influence na yeye hataki kufundishwa Tabia Mbayaa, na kuongeza kuwa eti hajaonana na Ray C karibu miaka mitano sasa
Nilipompigia simu Ray C kumuuliza kuhusu ishu hii alishindwa kufunguka kwasababu mama anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa hospitali.
Wataalam wa Mambo wanasema eti Ray C alimtafuta Tid eti ili amshawishi kuachana na Madawa, Kheeeee..... kwani TID anatumia?
Kwa watu wanaowafahamu wanadai wasanii hao wanajuana vizuri na eti Ray C alifanya jitihada nyingi kumtafuta TID lakini jamaa alikua hapokei simu.
Sikiliza Interview niliyofanya na TID

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.