Saturday, July 5, 2014

SHETA: HAJUTII KUWEKEZA MILIONI 25 KWENYE VIDEO YA KEREWA

 
Msanii wa Bongo flava Nurdin Bilal a.k.a Sheta baada ya kuwekeza karibu milioni 25 kwenye utengenezaji wa Video ya wimbo wa "Kerewa" aliyoifanya chini ya Director mkubwa Afrika "God Father" mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini, Sheta anasema hajutii pesa yake ama mtonyo wake kutokana na Ubora wa kazi yenyewe na pili hivi karibuni baada ya kurudi bongo aliitwa na kampuni ya Spice Mobile na wakaingia mkataba mnono na kampuni hiyo itumie video hiyo kibiashara hasa kwenye mitandao na Sheta akapewa milioni 10 kama Advance na baada ya hapo atapewa pesa nyingine baadae.

Sheta anasema alipewa ushauri wa kuwekeza kwenye video kutoka kwa msanii mwenzake (Diamond Platnumz) awali alikua mzito kwasababu alikua hajawahi kufanya hivyo baadae akajikaza kisabuni pamja nawadau wake na kukwea pipa kuelekea kwa mzee Madiba na matunda yake ameanza kuyaona mapemaaaaaaaa.

Enyoy Video ya Kerewa hapo chini

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.