Monday, August 11, 2014

PENZI LA DIVA NA GK KAMA BOMBAY

Penzi la Veteran wa bongo Flava Crazy GK na mtangazaji wa Clouds fm Diva loveness linaendelea kunoga tofauti na watu walivyokua wakitabiri, wawili hawa wanakaribia kufikisha mwaka mmoja kwenye mahusiano na hivi karibuni kupitia account ya Instagram Diva alipost video mbili moja ikimwonyesha Crazy Gk akiangua mapera mtini kwa ajili ya kumpatia mpenzi wake na nyingine Crazy Gk akila mishikaki kwenye kisahani, Mtu mmoja baada ya kuona video hizi akaandika nanukuu "Inaonekana wawili hawa wako karibu sana na wana enjoy maisha ya kawaida na ndiyo mapenzi ya kweli, na picha ambazo zinapostiwa na mastar wengi wakionekana kwenye mahoteli ya kifahari ni kama maigizo."
mimi binafsi aina hii ya mahusiano jumlisha clip hizi za video inanikumbusha movie za kidosi Bollywood kwani mara nyingi wapenzi wa kwenye movie hizi huwa wanakua karibu sana na maisha yao yanakua ya kawaida ila yenye furaha.

CRAZY GK NA DIVA WAKILA BATA LA MISHIKAKI


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.