Monday, January 12, 2015

Kuelekea Uchaguzi:Davina Awatahadharisha Viongozi na Wananchi!!

Mwigizaji mkongwe Halima Yahya ‘Davina’, amewatahadharisha viongozi mbalimbali wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchanguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani 2015 kuwa makini ili wasisababishe vurugu au uvunjaji wa amani.
Davina alifunguka hayo juzikati katika mahojiano maalumu na paparazi wa GPL ambapo alisema mwaka huu unakuja kukiwa na changamoto nyingi kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea hivyo viongozi na Watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka umwagaji wa damu.
“Huu mwaka mzito sana na tunaweza kufurahi lakini kumbe kuna baadhi ya viongozi wanapanga kufanya mambo ya ajabu, tumeona uchanguzi wa Serikali za Mitaa juzi mambo yalivyokuwa, viongozi na Watanzania wenzangu lazima tuwe macho na sisi wapiga kura tumpinge kiongozi yeyote atakayetaka madaraka kwa njia ya vurugu,” alisema Davina.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.