Tuesday, July 7, 2015
VIDEO: ALLY NIPISHE AKATAA ZAWADI YA GARI
Haijawahi kutokea lakini hivi ndivyo picha nzima ilivyokua, Wiki iliyopita mshindi wa Tuzo ya Kili Best Upcoming 2013 Ally Nipishe, alifunguka kuwa amewahi kulala Gerezani kwa miezi mitatu kutokana na kununua gari wizi bila kujua, Ally Nipishe alidai kuwa alimwagiza mwanadada mmoja wa zanzibar ambaye walikua wapenzi, gari hilo lilipokuja Dar na yeye kuanza kulitembelea kumbe gari lilikua linatafutwa ndipo alipokutana na wana usalama waliomkamata na kumfungulia kesi ya wizi, Story hiyo iliskika na Mwanadada mmoja muigizaji wa Bongo Movie anafahamika kwa jina la Bozi, aliguswa na kujitokeza kwa mwandishi wa habari Hii Soudy Brown, Bozi akatanagaza Nia ya kumfuta machozi Ally Nipishe kwa kumnunulia gari kutoka kwenye Yadi yoyote ila thamani haitozidi milioni 30,
siku ya pili yake Nikamvutia Wire Ally Nipishe na Team yake, wakafika hadi clouds sikuwaambia dhumuni la mwanadada yule, tukaelekea hadi kwenye yadi moja ya magari maeneo ya Kinondoni Manyanya, kufika pale nikampa nafasi Bozi afunguke ya moyoni na Ally akapewa nafasi ya kuchagua Gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya milioni 13 lakini katika hali ya kushangaza Msanii Ally Nipishe alichomoa Ofa hiyo, Tazama tukio zima lilivyokua kwenye Clip hiyo hapo chini:
Comments System
facebook