Weekend iliyopita Nilifanikiwa kuwa mmoja kati ya wageni waalikwa kwenye sherehe za kutimiza siku 40 za mtoto wa Diamond Platnumz, ilikua ni sherehe iliyohudhuriwa na watu zaidi ya 350, Ma star wa bongo flava na bongo movie pamoja na ndugu na marafiki wa famili hii, nilifanikiwa kupenya hadi room kwa Diamond, na kupiga story na msanii huyo pamoja na baby mama wake maarufu kwa jina la Zari the Boss Lady, kitu cha kwanza nikaomba kuonyeshwa Choo ama bafu lenye thamani ya milioni 70 Habari ambayo ilivuma sana kipindi mjengo huu unakamilika, kuingia nikakutana na vitu vya thamani vilivyonakshiwa na dhahabu kama sink, ndipo Diamond akatoboa siri ambayo nilikua siijui kuwa anapenda kupiga usingizi ndani ya choo hicho kilichopo ndani ya nyumba yake "State House" Diamond aliongeza kuwa akiingia eneo hilo anajiskia faraja sana hivyo huweka hukausha mtungi wa kuogea (bathtab) na kuweka mito kisha hujilaza na kuangalia Tv,
nilimwona Diamond akikausha mtungi huo na kuusafisha nikamuuliza Je huwa anafanya hivyo siku zote na hakuna mfanyakazi wa ndani? Diamond akajibu ndio yupo dada anayefanya shughuli hizo ndipo Zari akaingilia kati na kumlalamikia Diamond kwa kutomtaja yeye Zari kwani amekua akisafisha kila siku sikiliza sauti ya tukio zima lilivyokua hapo chini