Mkali wa miondoko ya afro pop,rap pamoja na dance AIKA MAREALLE maarufu kama AIKA anayeunda kundi la Navy kenzo pamoja na EMANUEL MKONO a.k.a NAHREEL,ameibuka na kuwataja wasanii ambao waliomu inspire mpaka kufikia uamuzi wa kufanya music
Msanii huyo alisema kuwa alianza kupenda muziki tangu alipokua shuleni,na moja kati ya wasanii ambao alikua anawasikiliza na kufuata nyayo zao alikua beyonce pamoja na eve .
“Yaah nakumbukuka niligundua kuwa nna kipaji cha kuimba kipindi nilichokua shule na nilisoma nje ya nchi of course so,nilipokua shule nilikua napenda sana kuimba nyimbo tena hasa za nje”
Pia aliendelea kwa kuwataja baadhi ya watu ambao waliomu inspire kuingia katika industry ya music
“Mmh kwanza nakumbuka nilikua nampenda sana beyonce na i remember one day tulikua na show as school bash na nilikua mmoja kati ya waliopangwa ku perform that day so after finish walikuja rafiki zangu wengi walinipongeza na kuniambia Daaah AIKA leo umefanya kitu utadhani BEYONCE alikua live on stage so since that day wakaanza kunita jina la BEYONCE mpaka tunamaliza shule” ALISEMA AIKA
Aliongezea kwa kuwataja wanamuziki wengine kama EVE kwa upande wa Hip hop.