Kocha wa zamani wa Simba, James siang’a amefariki dunia nyumbani kwake eneo la Bungoma nchini Kenya usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Siang’a alikuwa golikipa na baadaye akiitumikia timu ya taifa ya Kenya ambapo lishiriki katika kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1972 na baadae akawa meneja wa Kenya mwaka kuanzia mwaka 1999 hadi 2000.
Alizidi
kung’ara na kuingia nchini Tanzania ambapo alikuwa meneja wa Taifa
Stars mwaka 2002, pia amewahi kuwa kocha wa timu mbalimbali katika
ukanda wa Afrika mashariki kama Simba SC, Moro United na Express ya uganda .
Mashabiki wa Simba SC watamkumbuka zaidi Siang’a kama Kocha wa mwisho kutamba na Simba kwenye ligi ya mabingwa Afrika hadi sasa ambapo simba ilicheza na
Zamaleck na kuifunga goli moja kwa bila mwaka 2003 na kuivua ubingwa klabu hiyo ya Misri ambapo hakuna kocha
aliyevunja rekodi hiyo.