Baada ya kubanwa na Ndanda FC kwa kulazimishwa suluhu mkoani Mtwara,Yanga imejipoza kwa Majimaji kwa kuichapa magoli 3-0 kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Yanga iliandika bao la kwanza dakika ya 35 kipundi cha
kwanza likifungwa na Deus Kaseke akiunganisha mpira wa mkwaju wa penati
ya Msuva uliogonga mwamba.
Amis Tambwe amefunga magoli mawili,ambapo alifunga bao la kwanza lake
la kwanza dakika ya 75 baada ya golikipa wa Majimaji kupangua krosi ya
Msuva kisha Mrundi huyo akausukumia kambani kwa kichwa. Dakika 10 baadae
Tambwe alipachika bao lake la pili akiitendea haki krosi ya Juma
Mahadh.
Matokeo ya michezo mingine.
Ruvu Shooting 1-0 JKT Ruvu
Mwadui FC 2-2 Stand Unied
Ndanda FC 0-0 Kagera Sugar