Klabu ya Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo
katika kipindi cha juma moja imepoteza michezo yake tena ikikubali kufungwa na klabu ya Watford
kwa magoli 3-1.
Watford walikuwa wa kwanza kupata goli lilifungwa na Daryl Janmaat kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.Ila kiungo wa Watford Zuniga alifunga ikiwa imesalia dakika saba mchezo kukamilika kabla ya Deeney alifunga penalti katika muda wa ziada baada ya Marouane Fellaini kumchezea vibaya katika eneo la hatari.
Hii ni mara ya tatu mfulilozi kwa Manchester United kupoteza,ikishindwa
2-1 na Manchester City,baadaye ikapoteza 1-0 dhidi ya klabu ya feyenoord
ya Uholanzi katikati ya wiki katika kombe la bara Ulaya.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika Mshambuaji wa Manchester United,Paul Pogba ali-post ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwashukuru mashabiki wa United na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito hali ilipelekea mashabiki wengi kuponda ujumbe wa mshambuliaji huyo aliesajiliwa kwa kiasi cha $105m.
Miongoni mwa walitupa madongo kwa mshambuliaji huyo ni Mwanamuziki wa Bongo fleva,Madee Ali ambae ni shabiki wa Unite alie-coment kwa kuandika "U can wapi ww rudisha mapene ya watu..ww mtu gani ufungi..mbona xhaka kafunga jana".Aliandika Madee.
Swali la kujiuliza,kwa lugha aliyotumia Madee ujumbe utakua umefika kweli...!!!.