Monday, September 19, 2016

Mkongwe wa muziki wa "Kwaito",Mandoza afariki akiwa na miaka 38.

Kama umekua ukiufatilia muziki wa "Kwaito" ambao ni maarufu sana nchini Afrika Kusini,Jina la  Mduduzi Edmund Tshabalala,maarufu kama Mandoza litakua sio jina geni masikioni mwako.Ila kwa sasa mkongwe huyu anaetajwa kama miongoni mwa wnamuziki walioutangaza muziki wa "Kwaito" nnje ya Afika Kusini,hatunae  tena kwani familia yake ilithibitisha kifo chake jumapili ya Sept.19 baada ya kushambuliwa na  maradhi ya kansa aliyopambana nayo kwa muda mrefu.

 Image result for mandoza on stage
Mandoza ambae ni mzaliwa wa Cape Town alianza harakati zake za muziki kwenye kikundi cha Kwaito kilichofahamika kama Chiskop kilichowajumuisha marafiki zake wengine watatu.Hata hivyo kikundi hicho hakikupata mafanikio na manmo mwka 1999  Mandoza  alianza ku-release project zake kama msanii wa kujitegemea na kwa mara ya kwanza aliachia album yake iliyofahamika kama "9II5 Zola South".

Haikuishia hapo kwani mwaka 2000 aliachia album iliyofahamika kama  "Nkalakatha" album ambayo inatajwa kama album bora ya Kwaito kwa muda wote ambapo wengi wetu hapo ndipo tulipoanza kumfahamu kupitia album hiyo ambayo jina la album hiyo yaani "Nkalakatha" ilikua miongoni mwa nyimbo zilizowahi kuchezwa mara nyingi zaidi kwenye vituo vya redio na kumbi za starehe nchini Afika Kusini na nnje ya nchi hiyo na kupelekea singo hiyo kushinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka kwenye tuzo za "South African Music Awards" huku album hiyo ikifanikiwa kushinda tuzo za "SAMA" kama album bora ya muziki kwaito.


Mashabiki wa muziki wa "Kwaito" nchini Afrika Kusini,wanamuizki na watu maaarufu wamekua wakituma salamu za rambirambi na kuomboleza kifo cha Mkongwe huyo wa muziki wa Kwaito ambapo Rais Jacob Zuma ameelezea kifo cha Mandoza kama kupotea kwa miongoni mwa hazina kubwa kwenye jamii ya wanamuziki na mtu mwenye mchango mkubwa kwenye taifa la Afrika Kusini.

"South Africa has lost one of its pioneers whose music appealed to a cross section of our people‚ young and old and was known to have achieved the unique crossover culturally to be enjoyed by both black and white South Africans. It is a great loss to the nation and we wish to extend our deepest condolences to his wife Mpho‚ his family and hordes of fans"....."Mandoza will be sorely missed. May his soul rest in peace‚".Alisema Rais Zuma kwenye taarifa ya salamu za rambirambi kwenda kwa familia ya Mwanamuziki huyo.

Unaikumbuka "Nkalakatha",mtazame Mandoza aki-perfom live wimbo huu unaotajwa kama miongoni mwa hit's zake ambazo zilisumbua sana kwenye miaka ya 2000's.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.